Aunt lulu alazimisha penzi kwa Koffi Olomide

auntluluStaa asiyekaukiwa na vituko, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’.

Hamida Hassan

Staa asiyekaukiwa na vituko, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ ameonekana kulazimisha penzi kwa mwanamuziki Koffi Olomide kutokana na maelezo yake kwamba anampenda na atahakikisha anampata.

Akizungumza na Ijumaa baada ya Koffi kutua nchini kwa ajili ya shoo aliyoifanya Ukumbi wa Escape One jijini Dar, Anti Lulu alisema anampenda sana mwanaume huyo, amekuwa akifikiria jinsi ya kujisogeza kwake lakini anashindwa.

“Unajua nampenda sana Koffi, siyo kimuziki tu bali na kimapenzi. Niliwahi kumsikia akisema anapenda wanawake waliofungashia sasa nikiunganishwa naye unadhani atapindua kwangu. Yaani silali kwa sababu ya penzi lake,” alisema Lulu.

Toa comment