The House of Favourite Newspapers

Aunt Lulu apigwa stop na mama yake kujirusha!

0

auntlulu

NA MWANDISHI WETU

DAR ES SALAAM: Mrembo mwenye ‘taito’ ya utangazaji na uigizaji Bongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunt Lulu’ anadaiwa kupigwa ‘stop’ na mama yake kwenda kujirusha ovyo kwenye kumbi za starehe na mitaani kwani mzazi huyo amechoshwa na skendo zinazotolewa kila kukicha.

Sosi aliye karibu na mama huyo alisema kuwa, Aunt Lulu, baada ya kugombana na mpenzi wake, Bond Bin Suleiman kisha kurudi nyumbani kwao, mama yake alimpiga marufuku kwenda kujirusha na kuzurura ovyo mitaani bila sababu kwani amemvumilia mambo yake kwa muda mrefu.

“Unajua mama wa Aunt Lulu ameokoka, sasa kila kukicha maskendo yamekuwa yakimfikia na kumchosha hivyo ameamua kumtuliza nyumbani kwake na ana mpango wa kumfungulia sehemu ya kuuzia chakula ambapo atakuwa akiuza sanasana makanisani kwani kule anakoishi (Salasala), kuna makanisa kibao ya kilokole ambayo walokole wengi hushinda huko,” alisema mtu huyo.

Baada ya kupata ubuyu huyo, mwandishi wetu alimwendea hewani Aunt Lulu ambaye alikiri kutulizwa na mama yake nyumbani kwao, Salasala lakini akafunguka kuwa hata umri sasa unamsababisha atulie kwani mambo ya utoto ndiyo yalimfanya kucharuka.

Leave A Reply