AUNT MINYOOSHO KAMA YOTE !

BAADA ya kumwagana na aliyekuwa mzazi mwenzake, dansa Moses Iyobo, muigizaji Aunt Ezekiel amedaiwa kuachia mapichapicha mengi akiwa na mpenzi wake mpya kumnyoosha Iyobo.  Wambea wa Insta juzikati wametupia picha ya Aunt inayomuonesha akiwa na mpenzi wake huyo mpya kwenye ufukwe wakiponda raha ambapo wadau mbalimbali mtandaoni humo walikitafsiri kitendo hicho kuwa ni kumrusha roho Iyobo.

“Mh! Aunt minyoosho kama yote, mbona Iyobo atakoma sio kwa mapichapicha haya,” aliandika mdau mtandaoni. Hata hivyo wadau wengine walimtia moyo Iyobo kwamba apambane na hali yake kwani kama ni kuzaa, ameshazaa na mrembo huyo, aangalie ustarabu wake.


Loading...

Toa comment