The House of Favourite Newspapers

Aunt: ningetaka mtoto mweupe, ningezaa na mzungu

0

Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel akiwa na mzazi mwenzie pamoja na mtoto wao.

Na Imelda Mtema

Sawasawa! Katika kuonesha kuwa amechoshwa na manenomaneno, staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel ameliambia Ijumaa Wikienda kuwa watu wanaosema mwanaye Cookie ni mweusi ndiyo maana hamuoneshi, hawapo sawa kwani angetaka mtoto mweupe angezaa na Mzungu.

Akizungumza na gazeti hili wikiendi iliyopita, Aunt alisema kuwa kuna watu hawana kazi za kufanya bali kufuatilia maisha ya watu kila siku bila sababu za msingi kwa maana kumuonesha mtoto wake ni hiari yake na si kwa ajili ya watu.

“Hivi mpaka nilivyoamua kuzaa na Moo (Moses Iyobo), si nilimuona ni mweusi? Sasa kwa nini watu wanachonga, eti simuoneshi Cookie kwa vile ni mweusi, ningetaka mtoto mweupe si ningemtafuta Mzungu nizae naye?” aliwaka Aunt.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Leave A Reply