Aunty Lulu acharuka Bondi kuoa!

BAADA ya hivi karibuni mwigizaji wa filamu za Kibongo, Bondi Suleiman kufunga ndoa na mwanamama raia wa Burundi, Charlote Rafael, aliyewahi kuwa mpenzi wake wa kupika na kupakua, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ amecharuka vilivyo na kuhoji imekuwaje ameenda kuoa mwingine na siyo yeye.  Akipiga stori na Shusha Pumzi, Aunty Lulu alisema anajua Bondi ameoa ila anataka amrudishie vitu vyake alivyompa

kama kamera na kompyuta mpakato (laptop) pia ampeleke hospitalini akatibiwe jeraha alilompiga walipokuwa wapenzi na kumwachia kovu usoni ili lifutike.

“Bondi anirudishie laptop na kamera yangu haraka, kama hana hivyo vitu amwambie mkewe akamnunulie na kama kovu ampe mkewe pia siyo mimi, nataka sura yangu irudi kama ilivyokuwa, yaani kanitia doa halafu kaenda kuoa asiye na doa, hana akili kabisa huyu Bondi,” alisema Aunty Lulu kwa hasira. Alipotafutwa Bondi ajibu ‘mashtaka’ hayo hakupatikana hewani

STORI: MWANDISHI WETU


Loading...

Toa comment