Na Gladness Mallya| RISASI MCHANGANYIKO| Za Motomoto
BAADA ya hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutaja majina ya watu wanaohusishwa na madawa ya kulevya, msanii wa filamu Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu ’ amemng’ata sikio kiongozi huyo kumtaka kupanua wigo zaidi wa watuhumiwa hao.
Akipiga stori na Za Motomoto News, Aunty Lulu alisema licha ya kumuombea Mungu ampe ujasiri, busara na hekima, pia amemtaka Makonda kushughulika zaidi na wanaoingiza madawa hayo kuliko watumiaji.
“Kazi anayofanya Makonda ni nzuri lakini namshauri adili na wanaoingiza yaani hayo madawa yanaingiaje itakuwa njia rahisi kutokomeza ili kuokoa vijana ambao wametopea na kuathirika na matumizi ya madawa ya kulevya,” alisema.
Comments are closed.