The House of Favourite Newspapers

Aveva adaiwa kukwamisha usajili wa Mavugo

0

160Rais wa Simba, Evans Aveva.

Martha Mboma na Ibrahim Mussa
HAKIJAELEWEKA! Uongozi wa Klabu ya Vital’O ya Burundi, umemtupia lawama Rais wa Simba, Evans Aveva ukidai ndiye anayekwamisha usajili wa mshambuliaji wao Laudit Mavugo kujiunga na Simba.

Awali, ilidaiwa straika huyo alisajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili kazi iliyofanywa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Simba, Collins Frisch, kabla ya rais huyo kudaiwa kumuwekea ngumu kutokana na kuwa naye kwenye mkataba binafsi.

Mavugo aliyewahi kuzitumikia Polisi ya Rwanda na SC Kiyovu na kuwa na rekodi nzuri nchini Burundi, katika ligi ya msimu huu nchini humo, tayari amefunga mabao saba kwenye mechi saba alizocheza mpaka sasa.

Akizungumza na Championi Jumatatu moja kwa moja kutoka Burundi, Rais wa Vital’ O, Bikolimana Benjamini, alisema kuwa licha ya mazungumzo na Simba kufikia pazuri, wamekuwa wakikwamishwa na rais huyo kutokubali kwenda nchini Burundi kulimaliza suala hilo, badala yake anatuma watu wengine.

“Bado tupo katika mchakato kwa sababu katika kikao tulichokaa mwishoni wa wiki, hatukuweza kufikia muafaka kwani tulitegemea Rais wa Simba angefika hapa lakini amekua akituma watu tofauti na matarajio yetu ambapo tulikuwa tunahitaji afike mwenyewe licha ya kuwa tumekuwa tukiwasiliana kwa njia ya simu.

“Vital’O haiwezi kumzuia Mavugo kuja kucheza Simba isipokuwa Aveva ndiyo anakwamisha suala hilo yeye mwenyewe wala siyo sisi, naongea kama rais wa timu kuwa tupo tayari kumuachia, ni wao tu.

“Lakini tumepanga kuja huko Desemba 15, mwaka huu kwanza kuonana na Aveva kwa ajili ya suala hilo na kuweza kufikia muafaka kisha kuitembelea klabu hiyo kwa ujumla,” alisema Benjamini.

Leave A Reply