The House of Favourite Newspapers

Aveva, Kaburu Wampigia Magoti DPP

Mapema leo Ijumaa, Oktoba 11, 2019, katila Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupitia kwa wakili wa Serikali Wankyo Simon ameieleza kuwa aliyekuwa Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Kaburu wameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuomba kukiri makosa yao kutaka kuanza majadiliano ya namna ya kuimaliza kesi inayowakabili.

 

Wakili Wankyo ameiambia Mahakama kuwa washtakiwa wote wapo na Kesi ilipangwa kwa ajili ya kutolewa kwa uamuzi kuhusiana na hoja mbalimbali zilizowasilishwa na upande wa mashtaka kuhusu mahakama kuwaondolea mashtaka ya utakatishaji washtakiwa hayo.

 

Baada ya kuelezwa hayo,Hakimu Simba alisema bado hajamaliza kuandaa hivyo aliiahirisha Kesi hiyo hadi Oktoba 18, mwaka huu ambapo atautoa uamuzi huo.

 

Hatua hiyo ilifikiwa na upande wa mashtaka baada ya mahakama kuwaondolea mashtaka mawili ya utakatishaji, kati ya kumi yaliyokuwa yakiwakabili Aveva na Nyange baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka hayo dhidi yao.

 

Hata hivyo, washtakiwa hao pamoja na mwenzao Zacharias Hansppope walikutwa na kesi ya kujibu katika mashtaka saba ambayo ni kughushi, kula njama, matumizi mabaya ya madaraka, kutoa nyaraka za uongo, na kutoa maelezo ya uongo ambayo upande wa mashtaka uliweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

Comments are closed.