Aweso Amtumbua Meneja DAWASA Kinyerezi
Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemsimamisha Meneja wa DAWASA Kinyerezi Burton Mwalupaso Kwa kushindwa kutekeleza vyema majukumu yake ikiwa ni pamoja na kushindwa kujua Takwimu kamili za mahitaji ya Maji kwenye eneo hilo sambamba na malalamiko mengi ya wananchi.
Waziri Aweso ametoa maelekezo hayo Leo Julai 1, 2024 wakati akizungumza na Wananchi wa Tabata Kinyerezi katika ziara yake ya kukagua hali ya huduma ya maji katika Jiji la Dar es Salaam.
Awali Waziri Aweso alimuhoji Meneja huyo kutoa Takwimu za mahitaji ya Maji na uzalishaji katika Kata ya Kinyerezi ambapo awali alijibu kuwa Kata hiyo Ina watu takribani 62,304, huku mahitaji ya Maji yakiwa ni Lita 600,081 (Laki sita na themanini na Moja) kwa mwezi, na baada ya kuulizwa Tena akaeleza kuwa mahitaji ni Lita 22,704 Kwa siku, huku akishindwa kueleza namna alivyopata Takwimu hiyo.
Waziri Aweso Leo Julai 1, 2024 ameanza rasmi ziara ya kikazi katika mikoa ya huduma ya Maji inayotolewa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) akiwa na lengo la kufuatilia hali ya huduma ya Maji na kusikiliza changamoto za wananchi.