The House of Favourite Newspapers

Aweso: DAWASA, Hili Lisijirudie Tena!

0

WAZIRI wa Maji Maji Jumaa Aweso, ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa jitihada kubwa walizozifanya wakati wa changamoto ya upungufu wa maji jijini Dar es Salaam huku akiwataka kuharakisha mradi wa Kidunda na Rufiji.

 

Aweso ameyasema hayo jana alipokutana na Menejimenti ya Dawasa na kuwataka kuharakisha mchakato wa miradi hiyo ili adha ya maji katika jiji la Dar es Salaam isijirudie tena ikiwa ni pamoja na mradi wa Maji Kigamboni.

 

Mapema mwezi Novemba, jiji la Dar es Salaam lilikumbwa na adha kubwa ya uhaba wa maji na kupelekea kuwa na mgao kitendo ambacho kilimlazimu Aweso kutinga ofisi za Dawasa usiku wa Novemba 17 na kuwataka wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kufanya kazi usiku na mchana ili mfumo wa ugawaji maji unarejea katika hali yake ya kawaida.

 

“Nina kila sababu ya kuwashukuru na kuwapongeza kwa jitihada kubwa ambazo mlizifanya kipindi cha changamoto ya maji, mlifanya kazi usiku na mchana nakuhakikisha hali ya maji inarejea, naomba changamoto hii isijirudie tena, harakisheni miradi ya Kidunda na Rufiji ili hadha iliyojitokeza isijirudie” amesema Aweso.

 

Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema, utafiti wa mradi wa Bwawa la Kidunda umeshakamilisha ana ule wa Rufiji upo mbioni kuanza.

Amesema mahitaji ya maji ifikapo mwaka 2027 itakuwa zaidi ya bilioni moja hivyo mradi huo ni muhimu.
“Mradi wa Rufiji utakamilika na malengo yetu ukamilike kabla ya mwaka 2025 ili uzinduliwe na mheshimiwa Rais Samia,” amesema Luhemeja.

Leave A Reply