Azam FC: Kila Mtu Ashinde Mechi Zake

WAKIWApointi moja nyuma ya vinara Simba na Yanga kwenye vita ya kusaka ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Azam wamesema kwamba hawana presha yoyote, kinachotakiwa kwa sasa ni kila mtu ashinde mechi zake.

 

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Simba ni vinara wakiwa na pointi 61 wakicheza mechi 25, wakifuatiwa na Yanga wenye pointi 61 wakishuka dimbani mara 29, huku Azam ikishika nafasi ya tatu kwa pointi 60 zilizotokana na mechi 30.

Akizungumzia malengo yao, Nahodha wa Azam, Agrey Morris, alisema: “Tunashukuru Mungu kwa kasi ambayo kikosi chetu inayo hivi sasa, tulipitia kipindi kigumu hapo kabla na kurejea kwenye fomu hii ni jambo la kujivunia sana.

 

Tuko katika nafasi ya tatu na tofauti ya pointi moja pekee dhidi ya Simba na Yanga, licha ya wenzetu kuwa na michezo ya viporo, lakini niweke wazi kuwa, hatuna presha ya ubingwa, kinachotakiwa ni kila mtu ashinde mechi zake halafu masuala ya ubingwa yatakuja baadaye.”

STORI: JOEL THOMAS,Dar es Salaam


Toa comment