Azam Fc Kumkosa Dube Leo
WAWAKILISHI wengine wa Tanzania katika Kombe la shirikisho barani Afrika, Azam FC, leo, Jumamosi watakuwa kwenye dimba lao la kujidai la Azam Complex jijini Dar es salaam kumenyana na Horseed FC kutoka Somalia katika mechi ya awali ya kombe hilo.
Azam ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Horseed FC ambapo itamkosa mshambuliaji wake hatari, Prince Dube ambaye ni majeruhi.
Nyota huyo kwa sasa yupo nchini Afrika Kusini ambapo amefanyiwa upasuaji, uongozi wa Azam FC umeweka wazi kuwa maendeleo ya nyota huyo kwa sasa yanaendelea vizuri.
Dube ambaye msimu uliopita alitupia mabao 14 na kutoa pasi tano za mabao, atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita.