The House of Favourite Newspapers

Azam FC Wamruhusu Sure Boy Kusepa

0

KLABU ya Azam imemruhusu kwa moyo mmoja Kiungo wa Timu hiyo, Salum Abubakary ‘Sure Boy’ kuondoka kwenye klabu hiyo baada ya mchezaji huyo kugoma kuendelea kuwatumikia matajiri hao wa Dar es Salaam.

“Kuruhusiwa kwa SureBoy kuachana na Azam bila ya vikwazo si hasira ila ni hekima kutokana na huduma ya muda mrefu ya mchezaji huyo,” amesema Nassor Idrissa, Mwenyekiti Azam FC.

Haya yanajiri ikiwa ni siku chache baada ya Azam FC kuwarejesha Kikosini nyota wake watatu Aggrey Morris, Mudathir Yahya na Sure Boy waliokuwa wamesimamishwa kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu.

Nyota huyo anahusishwa kujiunga na miamba ya Jangwani Yanga SC na kwamba tayari ameshasaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia Wananchi wa Jangwani.

Leave A Reply