Azam FC Yamalizana na Kipa wa Kimataifa

 

GOLIKIPA wa kimataifa wa Uganda, Mathias Kigonya, amefuzu vipimo vya afya, tayari kujiunga na Klabu ya Azam FC akitokea Klabu ya Forest Rangers ya Zambia. Kigonya tayari ameshatua Bongo akitokea Uganda na kukamilisha utaratibu wa vipimo vya afya.

 

Kipa huyo anatarajiwa kupewa dili la mwaka mmoja kupambana ndani ya kikosi cha Azam FC ambacho kimeweka kambi ya siku 10 visiwani Zanzibar. Kupata dili kwa kipa huyu kunapoteza dili la kipa wa Biashara United, Daniel Mgore ambaye alikuwa anatajwa kuibukia ndani ya kikosi cha Azam FC.

 

Hii inatokana na kipa namba moja David Kissu ambaye alisajiliwa akiwa huru baada ya kuachana na Gormahia kufanya makosa ya mara kwa mara ambayo yameigharimu timu hiyo kupoteza pointi tatu katika mechi walizocheza.

 

Miongoni mwa mechi ambazo Kissu aliruhusu kufungwa ni pamoja na ile dhidi ya Yanga iliyosababisha Kocha Mkuu, Aristica Cioaba kufutwa kazi mazima pamoja na sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Biashara United.

 

Pia kwenye sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Ruvu Shooting, Kissu alionekana kurudia makosa yake jambo lilisababisha Azam FC wasake kipa.

Toa comment