The House of Favourite Newspapers

AZAM FC YATUA DAR KWA KISHINDO KUTOKA ZENJI

Nahodha wa Azam FC, Agrey Moris akiwa amenyanyua kikombe juu baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Zamani wakitokea Kisiwani Pemba

TIMU ya Azam FC imerejea jijini Dar es Salaam, mapema leo baada ya jana (Jumapili) kuibuka na ubingwa wa Mapinduzi Cup kwa mara ya tatu mfululizo katika mchezo wao dhidi ya Simba uliopigwa katika Uwanja wa Gombani Visiwani Pemba na kufanikiwa kuwachakaza Simba mabao 2-1.

 

Baadhi ya mashabiki wa Azam FC, wakishangilia baada ya timu yao kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa zamani mapema leo

Wakati huohuo,  wachezaji na benchi la ufundi la klabu ya Simba lililokuwa Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kushiriki michuano ya Mapinduzi wamerejea jijini Dar es Salaam, mapema leo kwa ajili ya kujiandaa na michuano mengine ambapo jana walipoteza mchezo wao wa fainali dhidi ya Azam FC,

Baadhi ya wachezaji wa timu ya simba wakiwasili katika uwanja wa ndege wa zamani wa JK
Meneja wa kikosi cha Simba B, Mussa Hassani Mgosi kushoto akiwa na mmoja wa wapiga picha wa ITV wakati akiwasili uwanjani hapo.

 

Wachezaji hao wakiweka mizigo yao kwenye gari tayari kwa kurejea makwao.

 

Comments are closed.