Azam Jipangeni, Aussems Ana Dawa Yenu

ZIKIWA zimebaki siku nane kabla ya Simba kuvaana na Azam FC kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara, bosi wa benchi la Simba, Mbelgiji Patrick Aussems ameweka wazi kwamba tayari ana dawa ya kushinda dhidi ya wapinzani wake. Kocha huyo ambaye ameiongoza Simba kukaa kileleni mwa ligi kuu wakiwa na pointi 12, atakuwa na kibarua cha kuiongoza Simba, Oktoba 26 kuvaana na Azam FC inayofundishwa na Mrundi Ettiene Ndayiragije.

 

Mara ya mwisho wakati timu hizo zilipokutana kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, Simba walishinda kwa mabao 4-2 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Aussems ameliambia Championi Ijumaa kuwa dawa hiyo ameipata baada ya kuangalia kwa umakini juu ya upungufu wa kikosi chake katika michezo ya kirafi ki ambayo wameicheza hivi karibuni.

“Nilikuwa naangalia baadhi ya vitu ndani ya kikosi changu kwenye mechi zetu tatu ambazo tumecheza za kirafi ki. “Kitu kikubwa ni kuwa kuna mabadiliko makubwa nimeyaona kwao japo sikuwa na wachezaji wangu wote lakini nilivyoviona naona kabisa vinatosha kuwa faida wakati wa mechi yetu na Azam.

 

“Wakati wote ambao tulikuwa tunacheza mechi zote hizi mawazo yangu yalikuwa kwa Azam FC nikifi kiria kwa namna gani tutapata ushindi kwao ila sasa tayari nimeshavipata,” alimaliza kocha huyo.


Loading...

Toa comment