Azam wapokea CV 10 za makocha kwa siku moja

MARA baada ya Azam kumvunjia mkataba kocha wake Mholanzi, Hans van Der Pluijm mapema juzi, imebainika kwamba uongozi huo tayari umepokea zaidi ya wasifu wa makocha 10 ambao wameomba kibarua kikosini hapo.

 

Azam FC, juzi Jumamosi walitangaza kuachana na Pluijm pamoja na msaidizi wake, Juma Mwambusi ikiwa ni baada ya timu hiyo inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu, kuwa na matokeo mabaya kwenye mechi zake tano zilizopita ikiwemo ya Simba. Lakini ndani ya siku moja tu, tayari wameshapokea wasifu ‘CV’ za makocha 10.

 

Makamu Mwenyekiti wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, amesema mara baada ya wao kuachana na Pluijm, tayari hadi jana walikuwa wamepokea ‘CV’ za makocha wapatao 10 ambao wanataka mikoba ya Mholanzi huyo ingawa kwa sasa timu ipo chini ya makocha wa muda, Meja Abdul Mingange na Idd Cheche kutoka timu za vijana za Azam. “Idadi inaongezeka tu kila mara lakini tukishakaa viongozi ndiyo tutaamua tufanye nini,” alisema Popat.

SAID ALLY, Dar es Salaam

MWINYI ZAHERA Aikana Azam Mapema tu


Loading...

Toa comment