The House of Favourite Newspapers

Azam Yamtimua Youssouph Dabo Kuanzia leo Septemba 3

0
Youssouph Dabo

BODI ya Wakurugenzi ya Azam FC na kocha, Youssouph Dabo, wamefikia makubaliano ya pande mbili ya kutoendelea kufanya kazi pamoja kuanzia leo Septemba 3, 2024.

Dabo aliyehudumu kwenye klabu hii kwa kipindi cha mwaka mmoja, anaondoka na wasaidizi wake wa benchi la ufundi aliokuja nao.

“Klabu pamoja na wadau wake inapenda kumshukuru Dabo kwa weledi na moyo wake wa kutokata tamaa katika kipindi chote alichokuwa nasi na tunamtakia kila la kheri huko
aendako” imesema sehemu ya taarifa ya Azam FC.

“Aidha, wakati bodi ikiwa kwenye mchakato wa kutafuta kocha mpya, programu za timu zitakuwa chini ya makocha
wa timu zetu za vijana”.

Leave A Reply