The House of Favourite Newspapers

Azam: Yanga mnawataka Tchetche, Wawa? Njooni

0

000Kipre Tchetche

Wilbert Molandi, Dar es Salaam
UONGOZI wa Azam FC umewajia juu mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga, juu ya taarifa kuwa wanawawania wachezaji wake kadhaa ambapo imewataka wafuate taratibu za kuwasajili kama kweli wana nia hiyo.

Kumekuwa na taarifa kuwa, Yanga ina mpango wa kuwasajili straika na beki wa Azam FC, Kipre Tchetche na Pascal Serge Wawa, wote raia wa Ivory Coast huku ikimuomba kwa mkopo kiungo, Mudathir Yahya.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, ameliambia gazeti hili kuwa hawataki kusikia klabu yoyote ikifanya mazungumzo na wachezaji wao katika kipindi hiki cha mapumziko.

“Kwa sasa wachezaji wetu wote wapo mapumzikoni, naziomba klabu ziache kuwasumbua wachezaji wetu katika kipindi hiki wakiwa wamepumzika.

“Wao kama wamevutiwa na baadhi ya wachezaji wetu wanatakiwa kuleta barua ofisini kwetu na siyo kuwafuata kinyemela na kutaka kufanya mazungumzo bila ya ruhusa ya uongozi.

“Isitoshe uongozi wa Azam hivi sasa upo tayari kumuachia mchezaji yeyote katika kujenga kikosi imara kitakachochukua ubingwa wa ligi kuu msimu huu,” alisema Kawemba.

Leave A Reply