Azam Yasuka Mipango ya Kuwamaliza Waarabu

BENCHI la ufundi la Azam FC limetamba kuwa kikosi chao kimejipanga vizuri kuhakikisha wanashinda mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramid inayoshiriki Ligi Kuu nchini Misri.

 

Azam wanatarajiwa kuanzia nyumbani katika mchezo huo wa hatua ya kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramid ambapo mchezo wa kwanza utapigwa Oktoba 16 kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

 

Azam walifikia hatua hiyo baada ya kuiondosha Horseed ya Somalia katika hatua ya awali kwa jumla ya mabao 4-1.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kocha Msaidizi wa Azam, Vivier Bahati, alisema: “Tumepoteza mchezo wetu uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania, licha ya kwamba tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga, hivyo tutarekebisha makosa yetu.

 

“Mchezo wetu unaofuata ni wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids FC ya Misri, tunajua utakuwa mchezo mgumu kwetu kutokana na ubora wa wapinzani wetu lakini tunaamini kikosi chetu kipo tayari kwa ajili ya mapambano, tutaanzia nyumbani, hivyo ni lazima tuhakikishe tunapata matokeo mazuri kabla ya mchezo wa marudiano ugenini.”

JOEL THOMAS NA MARIA RAYMOND, Dar es Salaam704
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment