The House of Favourite Newspapers

Azam Yazipa Simba, Yanga Sh 225.6 Bil

0

AZAM Media Limited jana, iliingia mkataba wa miaka 10 wa kurusha matangazo ya michezo ya Ligi Kuu Bara na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa kutoa kiasi cha shilingi bilioni 225.6.

 

Hii ni baada ya Azam kushinda zabuni ambayo ilitangazwa na TFF na wao kuwa na vigezo hivyo.

 

Mkataba huo mpya utaanza kufanya kazi msimu ujao wa 2021/22, huku kiasi hicho cha fedha kikimwagwa kwa timu za ligi hiyo zikiwemo Simba, Yanga na Azam.

 

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo, Rais wa TFF, Wallace Karia alisema matarajio yao nikuona ushindana unaongezeka msimu ujao.

“Hivi karibuni tulitangaza zabuni ya kumpata mzabuni atakayechukua haki ya kurusha matangazo ya mechi za ligi Azam imeshinda baada ya kutoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni shilingi bilioni 225.6, udhamini huo utakuwa wa kipindi cha miaka 10.

 

“Ni historia kubwa ya udhamini ambao imefanyika leo (jana), katika kipindi chote cha uongozi wa TFF, hivyo uongozi wangu umeweka historia kubwa, tumepanga kuandaa semina kwa viongozi wa klabu kwa lengo la kupata elimu, malipo ya fedha hizo yatafanyika kwa njia ya mtandao,” alisema Karia.

Mtendaji Mkuu wa Azam, Tido Mhando alisema: “Tangu mwanzoni dhamira yetu imekuwa ni kuendeleza soka la Tanzania kwa namna ya kipekee tunafarijika ambavyo tumefanikiwa katika kusaidia kuongezeka kwa kiwango cha soka letu.

 

“Kwa kuzingatia umuhimu wa ushindani wa thamani ya soka tumekubaliana asilimia 67 ya fedha za malipo ya kila msimu katika mkataba huu ziende kwa timu ambazo zinashiriki ligi kuu.

 

“Kwa msimu wa 2021/22, Azam Media itatoa shilingi billioni nane na sehemu ya fedha itakayosalia itasaidia maendeleo ya soka, TFF na Bodi ya Ligi Kuu.“Fedha hizo zitakuwa zikiongezeka kila msimu na ndiyo maana utaona msimu wa 2022/23, fedha zitakazotolewa ni shilingi billion 13.2, huku timu zikipata shilingi bilioni 8.8.“Misimu mitatu ijayo yaani 2021/22 mpaka 2023/24, bingwa wa ligi kuu atapata shilingi

Leave A Reply