The House of Favourite Newspapers

Aziz Ki Ashinda tuzo ya Mchezaji bora wa mwezi Machi 2024

0

Kiungo wa Yanga SC Stephen Aziz Ki ameshinda tuzo ya Mchezaji bora wa mwezi Machi kwa kuwashinda Clotous Chama wa Simba SC na Feisal Salum wa Azam FC ambao aliingia nao fainali.

Taarifa ya Bodi ya Ligi imeeleza kuwa Aziz Ki ameshinda tuzo hiyo kutokana na kuwa bora ndani ya mwezi March kwa kusaidia timu yake kushinda mechi tatu kati ya nne za Ligi Kuu Bara.

Aziz Ki alicheza jumla ya dakika 330 na amefunga magoli matatu na ametoa pasi za usaidizi wa magoli (assist) 4 (Yanga 5-0 Ihefu, Yanga 1-0 Geita, Namungo 1-3 Yanga na Azam FC 2-1 Yanga).

Leave A Reply