The House of Favourite Newspapers

Washindi wa Tuzo Za TFF 2023/24 Aziz Ki, FeiToto, Mzize, Shabalala Wabeba Tuzo Nne

0

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga Sc, Stephanie Aziz Ki ametangazwa kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara msimu wa 2023/24.

Aziz Ki iliibuka kinara wa upachikaji magoli akiingia kambani mara 21 magoli mawili mbele ya nyota wa Azam Fc, Faisal Salum ‘Feitoto’ aliyemaliza na magoli 19.

Nafasi ya tatu inashikiliwa na Wazir Junior (magoli 12), Saido Ntibanzokiza mwenye magoli 11 sawa na Maxi Nzengeli (magoli 11).

1. Mlinda mlango wa klabu ya Yanga Sc, Djigui Diarra ameshinda tuzo ya golikipa bora wa Michuano ya FA (CRDB FEDERATION CUP).

2. Ley Matampi ameshinda tuzo ya golikipa bora wa Ligi kuu ya NBC Tanzania bara

3. Beki wa Yanga Sc na Timu ya taifa ya Tanzania, Ibrahim Bacca ameshinda tuzo ya beki Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania

3. Aziz Ki raia wa Burkina Faso ameshinda tuzo ya kiungo bora wa Ligi Kuu

4. Nahodha wa mshambuliaji wa klabu ya Paok ya Ugiriki, Mbwana Samatta ameshinda tuzo ya Mchezaji bora wa kiume wa Tanzania anayecheza nje ya Tanzania.

5. Aziz Ki ameshinda tuzo ya mchezaji bora (MVP) wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania

6. Kiungo wa Azam Fc, Faisal Salum ‘Feitoto’ ameshinda tuzo ya mchezaji bora (MVP) wa kombe la Shirikisho la CRDB (CRDB Federation Cup 2023/24)

7. Mfungaji Bora CRDB Bank Federation Cup 2023/2024, Clement Mzize

Kikosi bora cha Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara 2023-24.
Lay Matampi (Coastal Union),
Kouassi Yao (Yanga SC),
Mohamed Hussein (Simba SC),
Ibrahim Bacca (Yanga SC)
Dickson Job (Yanga SC)
Feisal Salum (Azam FC)
Mudathir Yahaya (Yanga SC),
Kipre Junior (Azam FC), Aziz Ki (Yanga SC),
Maxi Nzengeli (Yanga SC) na
Wazir Junior (KMC).

Leave A Reply