Baada Ya Kuachana Na Travis Scott, Kylie Jenner Arudi Kwa Tyga

Baada ya siku chache kuenea kwa taarifa kuwa Kylie Jenner kuachana na mpenzi wake, Travis Scott sasa inasemekana kuwa amerudiana na mpenzi wake wa zamani Tyga

 

Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa mrembo Kylie Jenner alionekana akiwa anaingia hoteli ya Sunset Marquis ambayo ndani yake kuna studio za muzikiĀ  Tyga anafanya kazi zake humo.

Baada ya muda mfupi Tyga alionekana akitoka katika hoteli hiyo huku Kylie Mwenyewe akitoka kwa kutumia mlango mwingine kukwepa mapaparazzi.
.
Kylie Jenner na Tyga walikuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu kabla ya kuachana na Kylie Jenner kuwa na Travis Scott ambaye wamefanikiwa kupata mtoto mmoja, Stormi Webstar.


Loading...

Toa comment