The House of Favourite Newspapers

BAADA YA AKWILINA KUZIKWA, DENTI MWINGINE DAR AUAWA KINYAMA!

Shija Daudi Kasuku enzi za uahi wake.

 

WAKATI ripoti ya uchunguzi wa kipolisi juu ya mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafi rishaji (NIT), Akwilina Akwilini Bafta (22), ikizua gumzo kila kona kufuatia siku 14 za kuchunguza kutimia leo, tukio linguine la mauaji ya kutisha dhidi ya denti mwingine wa chuo kikuu limeshtua wengi.

 

Wakati Akwilina yeye aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa kwenye daladala maeneo ya Mkwajuni- Kinondoni jijini Dar, Februari 16, mwaka huu, mwanafunzi Shija Daudi Kasuku (20) wa Chuo Kikuu cha Elimu ya Biashara (CBE), Tawi la Dar, alidaiwa kuuawa kwa kusukumwa kutoka ghorofa ya tatu hadi chini.

 

Shija aliyekuwa akisomea Diploma ya Biashara akiwa yupo mwaka wa pili chuoni hapo, alidaiwa kuuawa na mwanafunzi mwenzake kwa kile kilichosemekana kwamba ni wivu wa kimapenzi.

 

Akiwa na marafiki zake.

 

SIMULIZI YA KUTISHA

Akisimulia tukio hilo la kutisha kwa majonzi, baba mzazi wa marehemu Shija, Daudi Shija Kasuku alisema kuwa, usiku wa Februari 26, mwaka huu, mishale ya saa nne, mke wake (mke wa baba wa marehemu) alipigiwa simu na mtu ambaye hakujitambulisha na kumuuliza kama yeye ndiye baba wa Shija?

“Alimwambia yeye siyo baba wa Shija bali ni mama wa Shija ndipo akamwambia kuwa motto wetu Shija amepata matatizo akiwa hosteli Ilala na amekimbizwa hospitalini (Amana).

“Tulivyopata ile taarifa tulishtuka mno, tukatoka mbio kuwahi katika Hospitali ya Amana (Ilala) tuliyotajiwa na yule mtu aliyetupatia taarifa.

 

WAPEWA TAARIFA MBAYA

“Tulipofi ka Amana tulikuta watu wamejaa. Wakati tukiwa hatuelewi nini cha kufanya, kuna mtu aliyekuwa akitufahamu ambaye alituita pembeni na kutupatia taarifa mbaya kuwa kijana wetu ameshafariki dunia. “Palepale tuliishiwa nguvu na kukosa la kufanya maana ni tukio la ghafla mno. Tulielezwa kuwa Shija alianguka kutoka ghorofa ya tatu hadi chini akiwa kwenye hosteli zao huko Ilala.

“Tuliambiwa alipasuka kichwani hivyo alikuwa anavuja damu mdomoni na puani,” alisema baba mzazi huyo kwa uchungu.

 

Baba huyo alisema kuwa, kutokana na tukio hilo, iliwalazimu kwenda Kituo cha Polisi cha Pangani, Ilala jijini Dar ambapo askari kituoni hapo waliwaeleza kuwa walikuwa na taarifa za tukio hilo na walikuwa wanalishughulikia.

 

Akwilina Akwilini Bafta enzi za uhai wake.

 

WAHUSIKA MBARONI

Alisema kuwa, walielezwa kuwa, wahusika wote wawili, yaanimwanafunzi wa kike aliyesababisha ugomvi na wa kiume aliyetuhumiwa kumsukuma mwenzake walishakamatwa kwa uchunguzi.

 

“Kwa mujibu wa maelezo ya askari, yule msichana aliwaambia alikuwa anaumwa pumu. Sasa, kwa kuwa Shija ndiye aliona ni mtu wa karibu wa kuweza

kumsaidia kwa muda huo,

alimwita na kumuomba

ampeleke hospitalini.

“Waliporudi kutoka hospitalini, wakawawamekaa wote chumbani kwa huyo msichana, Shija akiendelea kumtazama hali yake. “Baada ya muda ndipo akaingia mwanaume mwingine ambaye ilisadikika ni mpenzi wa huyo msichana.

 

SHIJA ASUKUMWA GHOROFANI

“Mara ilidaiwa kuwa huyo aliyedai yule msichana ni wa kwake, alianzisha ugomvi na Shija na kumsukuma kwa dirishani ndipo akaanguka hadi chini kutoka ghorofa ya tatu,” alimalizia kusimulia mzee huyo. Baba huyo alisema kuwa, baada ya uchunguzi wa polisi, Machi 3, mwaka huu, mwili wa marehemu utasafi rishwa kwenda Mwanza kwa mazishi.

 

 

 

Enzi za uhai wake.

 

RPC ILALA HUYU HAPA

Kwa upande wake, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ACP Salum Hamdani alipotafutwa kuhusiana na tukio hilo alisikiliza kwa makini maelezo ya mwandishi wetu na kusema kuwa, anafuatilia suala hilo. “Sijaletewa taarifa za hilo tukio mezani kwangu, lakini kwa kuwa umeeleza, ngoja nilifuatilie,” alisema Kamanda huyo.

 

RIPOTI YA AKWILINA

Kuhusu ripoti ya uchunguzi wa kipolisi juu ya mauaji ya Akwilina, Gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa ili kujua kinachoendelea ambapo simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi (SMS) haukujibiwa.

 

Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi wakati polisi wakizuia maandamano ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa wakielekea kwa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni kwenda kudai viapo vya mawakala wao kwa ajili ya uchaguzi wa marudio wa jimbo hilo.

 

Taaria za baadaye juu ya tukio hilo kutoka kwa Kamanda Mambosasa zilisema kuwa polisi sita walikamatwa kwa tuhuma za kutumia risasi za moto siku ya tukio la maandamano ya Chadema.

Comments are closed.