The House of Favourite Newspapers

Baada ya Coronavirus, Ugonjwa Mpya Hantavirus Waua China

0

RAIA mmoja China amefariki dunia baada ya kukutwa na virusi vya Hanta (Hantavirus) akiwa kwenye basi alipokuwa akielekea Shandong. Aidha watu 32 waliokuwa wamepanda naye kwenye basi wanafanyiwa uchunguzi wa virusi hivyo.

 

Kwa mujibu wa Kituo cha  Udhibiti wa  Uzuiaji wa Magonjwa   (CDC) cha Marekani, virusi hivyo ambavyo vinajulikana kama “New World” (Dunia Mpya) nchini Marekani, huenezwa na panya na husababisha magonjwa mbalimbali kwa watu kwa huathiri mfumo wa upumuaji.

 

Virusi hivyo huenezwa kutoka kwa wanyama kupitia hewa na hutolewa pia kupitia mkojo, kinyesi mate, na mara chache kwa kuumwa na mnyama wenye wadudu hao.

 

Hantavirus imetokea wakati China inakabiliana na Coronavirus iliyosababisha vifo vya watu 3,277 nchini humo hususani katika mji wa Wuhn jimbo la Hubei.

 

Matukio zaidi ya 386,350 yameripotiwa katika nchi 175 tangu ulipoanza nchini China.

Leave A Reply