#GlobalCelebrityUpdates: Baada Ya Davido Na Wizkid, Tekno Nae Adondosha Wino Na SONY Music.

Baada ya kufanya vizuri na single yake ya Pana, Tekno anazidi kupasua anga level za kimataifa. 

Mtandao wa Billboard umethibitisha taarifa zilizokuwa zinasambaa juu ya SONY Music kutaka kumsignisha Tekno kwenye lebo yao. Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa kwenye mtandao huo, staa huyo wa muziki kutoka Nigeria amesign mkataba mnono wenye thamani ya USD 4 Million na Colmbia Records kampuni inayomilikiwa na SONY Music

Tulivutiwa na Tekno baada ya kuusikia Pana ukisikilizwa na watu wengi Marekani, Uingereza na Canada, ila binafsi nilikutana na wimbo huo baada ya kuona video iliyokuwa iki-trend Facebook ya wapenzi wakiucheza wimbo huo beach. Niliusikiliza mara mbili mbili, nikaupenda, nikawaambia na watu wangu ofisini….” – Vice President na A&R wa Colombia Records Imran Majid aliiambia Billboard.

Kuna wasanii wengi wazuri wanaibuka kutoka West Africa, na muziki wao unakuja kwa kasi kubwa na kusikilizwa sana na watu Marekani, Uiingereza, Canada na karibia Ulaya nzima ” – Imran Majid.

Mkataba wa msanii huyo upo tofauti kidogo na mikataba waliosign Wizkid na Davido, mkataba wa Tekno na Colombia Records ni wa kurekodi nyimbo tatu zitakazo simamiwa na Colombia Records, SONY Music na kusambazwa kwenye soko la kimataifa ikiwemo Marekani yenyewe, Uiingereza, Canada na sehemu nyingine duniani, lakini dili hilo haitomzuia Tekno kurekodi au kutoa nyimbo kwa mashabiki wake wa Africa.

Tekno ana team ya watu wazuri na wanaomsimamia vizuri kwenye soko la muziki Africa, hivyo anaweza kuendelea kwa wakati wowote kurekodi au kuachia nyimbo kwa ajili ya watu wake wa nyumbani na Africa kwa ujumla, ila kwa upande wetu, sisi tutaweka nguvu nyingi zaidi kwenye kuusogeza wimbo wa Pana kwa wasikilizaji wengi zaidi wa huku.” – Majid aliiambia Billboard.

Kwa mujibu wa mtandao wa Pulse.ng wa Nigeria, single ya ‘Pana’ sasa ni mali rasmi ya SONY Music na Tekno atatakiwa kurekodi tena nyimbo nyingine mbili chini ya Colombia Records, nyimbo hizo zitazingatia vigezo vilivyo orodheshwa kwenye mkataba wao na perfornace ya nyimbo hizo ndio zitaweza kuishawishi lebo ya Colombia Records kuongeza mkataba wao na Tekno au kuishia tu na nyimbo walizokubaliana.

Imeandikwa Na: Sandra Brown

Source: Billboard/ Pulse.ng


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment