The House of Favourite Newspapers

Baada ya Hawa Simba SC Yatua kwa Zungu

0

Ammy Ali

Ame Ali ‘Zungu’.

Mohammed Mdose na Hans Mloli
Baada ya kuelezwa kuwa imesajili majembe kadhaa Simba ipo kwenye uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Azam FC, Ame Ali ‘Zungu’.

Tayari Simba ilishafanya uangalizi wa mastraika mbalimbali kwa ajili ya kuja kuisaidia timu hiyo lakini makubaliano ya kumshusha Zungu kikosini hapo yaliafikiwa kwenye kikao cha hivi karibuni cha baadhi ya viongozi wanaohusika na usajili.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa tayari kuna mazungumzo ya chini baina ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar na vigogo hao na kwamba yameonekana kwenda vizuri.

Licha ya uwezo wa kupambana anapokuwa uwanjani lakini kingine kilichowashawishi vya kutosha Simba kumuhitaji fowadi huyo ni suala la nidhamu yake kuanzia ndani mpaka nje ya uwanja. “Ame naye yumo kwenye listi ya watu ambao tumeona wanaweza kutusaidia msimu ujao, unajua nidhamu yake na hata aina ya soka kulingana na Simba ilivyo anaweza kuwa msaada mkubwa hapa, lakini bado ishu haijakamilika maana ni suala la umakini zaidi katika maamuzi,” kilisema chanzo kutoka klabuni hapo.

Pamoja na hayo, alipotafutwa Ame kuhusiana na ishu hiyo, alisema: “Hapana sijazungumza na Simba wala timu yoyote mpaka sasa juu ya kuhitaji kunisajili, nipo mapumzikoni Zanzibar kwa muda mrefu na bado sijapata taarifa hizo.”

Hata hivyo, Simba inayoelezwa kufanya usajili wake kwa siri mno imetajwa kuwa imeshamalizana na Hamad Juma wa Coastal Union, Mzamiru Yasin (Mtibwa Sugar), Jamal Mnyate na Emmanuel Semwanza (wote wa Mwadui FC).

Leave A Reply