The House of Favourite Newspapers

#GlobalUpdates: Baada Ya Instagram Na WhatsApp, Facebook Nao Waja Feature Mpya Ya ‘Facebook Stories’

Kampuni ya Facebook inazidi kukoleza moto vita yake dhidi ya Snapchat. Baada ya kuisogeza ‘stories’ kwenye Instagram na WhatsApp, kampuni hiyo imeamua kuileta feature hiyo kwenye App yao.

Siku ya Jumanne Machi 28 2017, Facebook ilizindua rasmi ‘Facebook Stories’ feature mpya inayofanana na Snapchat ambayo pia inaitwa ‘Stories’ inayowaruhusu watumiaji wa Facebook kushare picha na videos zinazopotea baada ya masaa 24. Kwa mujibu wa mtandao wa CNet, Facebook wamefanya maamuzi hayo baada ya kuijaribu feature hiyo kwa watumiaji wa Marekani, Ireland na Chile na kuona feature hiyo inatumika na zaidi ya watu billion 1.7  kwa mwezi.

Facebook Stories ni feature iliyotokana na wazo la Snapchat Stories na tumeona wamefanya kazi nzuri kuishawishi dunia nzima kuwa feature hiyo ni moja ya njia ambazo watumiaji wa mitandao ya kijamii hupenda kutumia ku-share picha na videos zao kwenye mitandao hiyo…” – Alisema Connor Hayes Product Manager wa Facebook kwenye press conference iliyofanyika Jumatatu hii jijini San Fransisco.

Facebook Stories inakuruhusu kupiga picha na kuweka video nyingi utakazo zinazopotea baada ya masaa 24, licha ya hayo feature hiyo pia inakuruhusu kuweka filters na masks uzipendazo kwenye picha ama video zako.

Kwa taarifa zaidi juu ya Facebook Stories, gusa hii link ya blue.

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Source: Facebook Newsroom.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

 

 

Comments are closed.