The House of Favourite Newspapers

Baada ya kifo cha Sir Chande BOSI MPYA FREEMASON BONGO ashangaza

MASHARTI ya kumuona bosi mpya wa Jumuiya ya Freemason Tanzania na Afrika Mashariki ambaye amechukua mikoba ya aliyekuwa kiongozi kabla yake, marehemu Sir Andy Chande yanashangaza na kuibua maswali.

Sir Andy Chande ambaye jina lake rasmi ni Sir Jayantilal Keshavji Chande KBE aliyefariki dunia Aprili 7, 2017 akiwa na miaka 89, alikuwa maarufu kwenye jamii hiyo kwa miaka mingi, tangu enzi za utawala wa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na alihudhuria shughuli mbalimbali za kitaifa na kijamii.

Waandishi wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Ijumaa iliyopita waliamua kufunga safari hadi zilipo ofisi za jumuiya hiyo, Posta jijini Dar kwa lengo la kumfahamu kiongozi mpya na kufanya naye mahojiano.

Mapaparazi wetu walipokelewa vizuri na mlinzi wa zamu aliyekuwa getini, ambapo kwanza walijitambulisha kisha wakaeleza nia yao ya kwenda hapo. “Kwa leo hamuwezi kumuona,” alijibu kwa kifupi mlinzi huyo ambaye alikataa kutaja jina lake.

Ijumaa Wikienda: Hayupo ofisini au ametoka? Tuna umuhimu wa kuzungumza naye.

Mlinzi: Siwezi kusema kama yupo au hayupo, lakini muhimu ni kwamba hamuwezi kumuona leo, kwa sababu siyo ratiba yake.

Ijumaa Wikienda: Kwani ratiba ikoje?

Mlinzi: Ratiba ya wageni wote kuonana na bosi ni Jumatatu tu, muda ni kati ya saa 12:00 jioni hadi 7:00 usiku. Vinginevyo haiwezekani, hata akiwepo ofisini nje ya muda na siku hiyo moja tu ya Jumatatu haiwezekani kumuona.

Ijumaa Wikienda: Huyo bosi wenu mpya anaitwa nani?

Mlinzi: Dah! Jamaa jina lake gumu sana…ni Mhindi na hawa watu bwana majina yao mimi huwaga yananishinda sana kuyataja.

Ijumaa Wikienda: Mtu akitaka kujiunga na Freemason, masharti yake yakoje?

Mlinzi: Mimi sijui maana siyo mwanachama. Mimi ninafanya kazi hapa, nimeletwa na kampuni yangu ya ulinzi kama unavyoona (anaonesha sare zake za kazini).

Ijumaa Wikienda: Mbali na Freemason, watu wengine huwa wanakodisha ukumbi hapa kwa ajili ya mikutano yao?

Mlinzi: Hapana, hapa ni wenyewe tu. Huku ndani kuna ukumbi mkubwa ambao unatumiwa na wanachama wa Freemason kwa ajili ya kufanya mikutano yao na kuondoka, lakini bosi yeye ana ofisi yake kabisa hapa hapa.

Ijumaa Wikienda liliondoka eneo la tukio likiahidi kurejea tena katika siku na tarehe iliyotajwa, lakini likiwa na maswali mengi kuhusiana na ratiba hiyo ya kushangaza.

Tunawaahidi kuwaletea mahojiano yetu na mkuu huyo mpya wa Freemason mara baada ya kuyakamilisha

Comments are closed.