The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kifungo, Meek Mill Aiangukia Mahakama

0

Meek-Mill-Main-Pub-1-James-Dimmock

Philadelphia, Marekani

Meek Mill ambaye ni rapa maarufu kutoka Philly nchini Marekani amabye anatumikia kifungo cha nyumbani cha miezi mitatu (siku) amabacho hatakiwi kujishughulisha na kazi yeyote ya muziki kwa muda wote wa kifungo change, kupitia mwanasheria wake Joe Tacopina ‘anakomaa’ kukata rufaa ili kuomba apunguziwe adhabu hiyo aliyohukumiwa mwezi uliopita baada ya kukiuka masharti ya kifungo chake cha awali.

Meek anaomba apunguziwe adhabu hiyo ili aweze kuendelea kufanya kazi za muziki katika studio yake ambayo ametengeneza nyumbani kwake.

Jaji wa Philadelphia alimpatia Meek adhabu ya miezi 6 hadi 12 kutokutoka ndani ya nchi hiyo, atafanya kwa muda wa siku zisizopungua 90 na hatoruhusiwa kujishughulisha na kazi yeyote ya muziki ikiwemo kurekodi, kufanya shoo na nyingine kama hizo badala yake kufanya kazi za kijamii.

Jaji huyo atafanya matazamio ya adhabu hiyo baada ya siku 90 ili kuamua ni muda gani ataendelea kubakia kwenye kifungo hicho.

Mbali na adhabu hiyo meek yupo kwenye muda wa matazamio kwa miaka 6 kutokana na mwendelezo wa makosa yake.

Leave A Reply