The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Baada ya Kuachiwa Huru, Hii ni Sentensi ya Lema kwa Rais Magufuli

MBUNGE wa Arusha Mjini kwa Tiketi ya Chadema, Godbless Lema leo Machi 3, 2017 ameachiwa huru na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwa dhamana ya milioni 1 huku akipewa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaokidhi vigezo kwa mujibu wa sheria.

Mbunge Lema aliyesota mahabusu kwa takribani miezi minne akikabiliwa na kesi ya uchochezi, katika Gereza Kuu la Arusha lililopo Kisongo, hatimaye amepata dhamani na kupokewa kwa mbwembe na washabiki wake waliomtandikia kanga ili apite wakati akitoka mahakamani hapo.

Mara tu baada ya kuachiwa huru, Lema amesema kuwa ameandaa Walaka Maalum kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu mateso wanayoyapata watu waliyoko mahabusu na kwamba atautoa siku za hivi karibuni.

Nisikusimulie mengi, bofya Play umsikie Lema mwenye akizungumza.

Comments are closed.