The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kuibuka Kwa Sakata la Uuzwaji wa Hisa  za Tanga Cement kwa Twiga Cement,Wadau Wa Maendeleo Wahoji

0
UKWELI ni kwamba baada ya kuibuka kwa sakata la uuzwaji wa hisa  za Tanga Cement kwa Twiga Cement kumeendelea kuibua hoja mbalimbali kwa baadhi ya wadau wa maendeleo ya viwanda ambao wameendelea kuhoji pande mbalimbali ambazo hazijawahi kusikika hapo awali,
Ambazo zilifanikiwa kukata rufaa 19 na rufaa za HARAKA ni miongoni mwa nyingi zilizokatwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania ya Ushindani wa Haki.
Baadhi ya wakataji rufaa hao wamewahi kuipeleka Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mahakamani na baadhi ya rufaa hizo, walalamikaji ndio pekee waliokuwa wakitoa hoja zao.
 Sio Heidelberg / Twiga wala Tanga, rufaa  nyingi tayari zilitupiliwa mbali na Mahakama kutokana na kutokuwa za kweli.
Kutokana na mazingira hayo, mmoja wa makarani wa Mahakama ambaye hakutaka jina lake litajwe wala kuandikwa ameeleza anamashaka ya kuwa malalamiko mengi ni nakala za yale ya awali ambayo tayari yalishawasilishwa, hali ambayo inaibua mashaka kuhusu makundi hayo kuwa ni yaleyale ya awali ambayo kwa sasa yanatumia majina mengine.
Pia ikumbukwe kuwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara alionesha uthibitisho kwamba kampuni hiyo inayodaiwa kuwa mkoani Pwani inaonekana ilidanganya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).
Inawezekana  makundi hayo ya siri yanaweza kueleza uongo kwa FCT na mahakamani pia walianzisha mashambulizi mengine kupitia vyombo vya habari. Kampeni yao ni ya makusudi na ya kueneza habari potofu.
Cha kusikitisha ni kwamba michezo hiyo inaleta madhara makubwa kwa uchumi wa nchi yetu ambayo  viongozi wetu wanapambana zaidi kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi endelevu.
Kwa bahati mbaya zaidi taswira yetu machoni pa wawekezaji wa kimataifa kampeni zao za kipropaganda ambazo zilipotosha hata wabunge wetu kadhaa hata hivi majuzi.Swali la msingi la kujiuliza sasa makundi kama hayo yanawezaje kuendelea kuumiza uchumi wa  nchi yetu?
Leave A Reply