The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kukoswa ubunge… Afande Sele aburuzwa kortini

0

AFANDE SELE1Aaliyekuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini kwa leseni ya chama cha ACT- Wazalendo, Seleman Abdallah Msindi ‘Afande Sele’.

Dustan Shekidele, Mororogoro

ALIYEKUWA Mgombea Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini kwa leseni ya chama cha ACT- Wazalendo, Seleman Abdallah Msindi maarufu kama Afande Sele, ameburuzwa mahakamani akidaiwa kutapeli fedha zilizotokana na kuchapishiwa fulana zilizotumika wakati wa uzinduzi wa kampeni zake Septemba 14, mwaka huu.

afandeszzHellen B Massawe

Mwanasiasa huyo ambaye pia ni msanii mkongwe wa Muziki wa Kizazi Kipya, amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo Chamwino akidaiwa kutomlipa mjasiriamali Hellen B Massawe kiasi cha shilingi 1,390,000.

Hellen ambaye ni mkazi wa Dar es Salaam, aliliambia gazeti hili akiwa nje ya ofisi za chama hicho mjini Morogoro kuwa alikopa benki na kufanya kazi ya kutengeneza fulana hizo kwa wanasiasa wa vyama vingi, lakini ni Afande Sele pekee ambaye hakumlipa na kila alipomfuata alimtaka kufuata fedha hizo kwa kiongozi mkuu wa chama, Zitto Kabwe.

AFANDE SELE11 Hati ya kuitwa

“Baada ya kuzunguka huku na kule bila mafanikio, hasa baada ya kuambiwa kuwa chama kisingeweza kumpa fedha kwa vile mgombea huyo alishapewa ruzuku, aliamua kwenda mahakamani kufuatia ushauri wa polisi kuwa hiyo ni kesi ya madai. Nimeenda mahakamani na nikapewa samansi ambayo Afande Sele ameisaini,” alisema.

Afande-SeleKatika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu, Aziz Abood alishinda Ubunge Jimbo la Morogoro mjini kupitia CCM huku mgombea wa Chadema, Marcossy Albani akishika nafasi ya pili na Afande Sele aliambulia nafasi ya tatu.

Leave A Reply