The House of Favourite Newspapers

BAADA YA KUMPA JEURI YA FEDHA KIGOGO AMMWAGA LULU DIVA

DAR ES SALAAM: MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ anadaiwa kuwa katika wakati mgumu baada ya kigogo (jina hapendi kumtaja) aliyekuwa akimpa jeuri ya fedha mjini kudaiwa kummwaga.

Chanzo makini kilieleza kwamba, kigogo huyo alimwagana na Lulu Diva hivi karibuni japokuwa mwanadada huyo amekuwa akifanya kuwa ni siri kwani anahofia watu ‘watamzodoa’ kwa maneno endapo wakiujua ukweli.

“Yule kigogo aliyekuwa anampa jeuri Lulu Diva amemmwaga na amemnyang’anya mpaka lile gari la kifahari alilokuwa anajidai nalo mjini, sasa sijui itakuwaje na ataishi vipi maana ameshazoea kujishaua nalo,” kilisema chanzo.

Ili kuujua ukweli, Amani lilimtinga nyumbani kwake Lulu Diva maeneo ya maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar ambapo lilipomkuta, alifunguka kuwa kigogo huyo hajammwaga ila wamemwagana na yeye kama mwanamke ameamua kujiongeza kwa sababu mpenzi wake huyo hakuwa muaminifu. “Yaani unajua kuna kipindi kingine mwanamke unapaswa kujifunza kujiongeza mwenyewe ndiyo moja ya mafanikio yako. “Siyo kila wakati umtegemee mtu akuongoze kwenye maisha yako kitu ambacho kimepitwa na wakati na ndiyo maana nikaamua kuendelea na maisha yangu na kupiga kazi tu,” alisema Lulu Diva.

VIPI KUHUSU GARI, NYUMBA ALIYOPANGIWA?

Akifafanua kuhusu gari la kifahari aina ya Jeep Wrangle lenye thamani ya shilingi milioni 90, alilonunuliwa na kigogo huyo kuwa amenyang’anywa, Lulu Diva alisema gari hilo analo na hajalichukua.

“Gari bado ninalo, kuhusu nyumba si ndiyo unaona bado ninaishi hapahapa jamani? Nitaendelea kukaa hapa maana nina uwezo wa kulipa kodi kupitia muziki wangu,” alisema Lulu Diva. Licha ya kusema gari hajanyang’anywa, siku hiyo mwandishi wetu alipojaribu kuangaza macho nyumbani hapo, hakuliona gari hilo.

Comments are closed.