The House of Favourite Newspapers

Baada ya kumtungia wimbo siri ya harmonize kwa jpm yaanikwa!

IMEISHA hiyo! Ndivyo unavyoweza kusema kwa lugha nyepesi baada ya kuanikwa kwa siri ya staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’ kumtungia wimbo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’.

TUJIUNGE

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Harmonize aliachia Wimbo wa Magufuli ukiwa ni Remix ya Wimbo wa Kwangwaru ambao ndani yake amesifia mema mengi ya kimaendeleo ambayo ameyafanya Rais Magufuli ambapo katika video yake ameonesha vitu mbalimbali alivyofanikisha tangu ameingia madarakani.

Mara baada ya kuachiwa kwa wimbo huo, mapokeo yake yamekuwa tofauti huku mashabiki wengi wakiwa hawaamini kama msanii huyo ambaye pia ni memba kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) angeweza kuibuka na kuimba hivyo.

”Ni jambo ambalo halijawahi kufikiriwa wala kufanywa na msanii yeyote wa Bongo Fleva kwa miaka ya hivi karibuni, lakini Harmonize ameweza kufanya, kiukweli ameweka rekodi ya aina yake,” ilisomeka moja ya komenti mtandaoni.

HARMONIZE AIBUKA

Hata hivyo, wakati hayo yakiendelea, Harmonize kupitia ukurasa wake wa Instagram alianza kuposti baadhi ya picha zikimuonesha Rais Magufuli na kuandika maneno ya kumsifia. “Hebu leo tuzungumze ‘serious’ kidogo, ndugu zangu hili suala linahusu maendeleo ya taifa letu ambalo manufaa yake ni kwa faida ya vizazi na vizazi…!!

“Ukiwa kama Mtanzania wa kawaida…Ni kitu gani unachojivunia katika utendaji wa Serikali yetu ya Awamu ya 5? Au ni kitu gani ambacho Rais wetu mheshimiwa John Pombe Magufuli amekifanya unatamani siku moja ukipata nafasi ya kukutana naye umwambie au umpongeze?”

Haikuishia hapo, mkali huyo aliposti tena na kuandika; “Naomba niseme kwa heshima na taadhima nikiwa kama Mtanzania mzalendo niliyezaliwa Mtwara, ninaipongeza sana Serikali ya Awamu ya 5, lakini pia nichukue fursa hii kuzishukuru Serikali za awamu zote tukufu zilizopita kwa misingi mizuri ambayo tunajivunia sisi na vizazi vijavyo!!”

Harmonize hakuishia hapo, alieleza siku ya kwanza alipoanza kuandika mashairi ya wimbo huo;

“Ile naanza kuandika tu laini ya kwanza niko studio mara mwanangu @chopa_the_bestboy akaingia, akaguna!!!! Sijakaa vizuri meneja wangu @ mjerumani_255 ikabidi achomoke ofisini kwake, akaja kuniambia hii ni zawadi tosha anayostahili Rais Magufuli, hebu imalize haraka! Basi ile namalizia tu @jembenijembe huyooo! Akaniambia mdogo wangu hii isiende audio tupu, lazima Watanzania wachache wanaojitia hawayaoni mazuri ya Rais wetu wayaone kwa macho!

“Basi akaanza kufanya harakati kupiga simu maeneo kadhaa, jioni ananiambia tunachukua video kesho yake, kama masihara asubuhi akaniamsha mapema, nikaungana na @director_ kenny tukafanya yetu.”

SIRI YAANIKWA

Mara baada ya sintofahamu kuenea huku msanii huyo akiweka posti na maneno ya kuisifia Serikali ya Magufuli, Gazeti la Ijumaa Wikienda lilimtafuta Harmonize ambapo alielekeza majibu yatolewe na meneja wake, Beauty Mmari ‘Mjerumani’.

“Hayo yote atazungumzia meneja wangu,” alisema kwa kifupi.

Baada ya kutafutwa Meneja Mjerumani alianika mengi ikiwemo siri ya Harmonize kumtungia wimbo JPM.

Ijumaa Wikienda: Kwanza niwapongeze kwa projekti mpya ya Harmonize ya Magufuli.

Mjerumani: Asante sana!

Ijumaa Wikienda: Labda ungetuambia, hamkupata pongezi yoyote kutoka serikalini kwa sababu imeongelea mambo mengi mema ya serikali?

Mjerumani: Watu wengi mno wameonesha kuufurahia na wengine wameguswa

sana, lakini pia hata viongozi wakubwa kwa namna moja au nyingine nimeona wameposti katika mitandao.

“Pia tunapokea simu nyingi kutoka kwa viongozi mbalimbali, naona ni kitu ambacho kimeigusa jamii moja kwa moja.

Ijumaa Wikienda: Nini siri ya wimbo huu?

Mjerumani: Unajua Harmonize ni msanii ambaye ni mbunifu sana! Anapenda utofauti na kama unavyojua wimbo wake wa Kwangwaru umefanya vizuri sana sokoni (una views (watazamaji) milioni 49 YouTube) na ni wimbo ambao bado upo sokoni kwani hata kwenye shoo zake ataimba nyimbo zote, lakini bila Kwangwaru shoo itakuwa haijaisha.

Akaona ili wimbo huu uweze kuishi sokoni, auelete kwa mtindo wa kijamii na hii inafanya Kwangwaru iendelee kuishi.

Ijumaa Wikienda: Mlishafikiria kuufikisha moja kwa moja kwa Rais Magufuli na nini siri ya Harmonize kumuimbia?

Mjerumani: Kwanza tumeutoa kama zawadi kwa Rais wetu ndiyo maana hatukufikiria kumshirikisha moja kwa moja Rais Magufuli, tulitaka auone kama sapraiz, lakini pia siri ya kumuimbia ni ajue kabisa kuwa vijana wake wasanii wanaifikiria Serikali na kuna vitu wanafuatilia bila Serikali kujua.

Ijumaa Wikienda: Ilikuwaje mkapata ruhusa kuchukua video baadhi ya maeneo kama vile jengo la tatu la abiria (Terminal III) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar, wakati wasanii wengine ni ngumu kupata?

Mjerumani: Tuliomba kibali kawaida tu kwenye mamlaka ya usimamizi wa viwanja vya ndege kwa hapa Dar tukaruhusiwa kuingia na kuchukua vipande vya video.

Comments are closed.