The House of Favourite Newspapers

Baada Ya Kurudi Kambini… Mbrazil Simba Atangaza Balaa Zito

0
Kikosi cha timu ya Simba

BAADA ya kumaliza mapumziko ya siku nne na kikosi chake kurejea rasmi kambini, Kocha mkuu wa Simba, Mbrazil Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ameweka wazi kuwa wapo saiti wakiandaa timu bora ambayo itashindania taji katika mashindano watakayoshiriki msimu ujao.

Kikosi cha Simba baada ya mapumziko ya siku nne, Jumatano hii walirejea kambini kwa ajili ya kuanza maandalizi ya michezo yao miwili iliyosalia ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union na baada ya hapo watakuwa wamefunga hesabu za msimu huu wa 2022/23 na kuanza kujiandaa na msimu mpya wa 2023/24.

Kuendana na ratiba ya Simba baada ya ushindi wao wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting, mchezo unaofuata utakuwa dhidi ya Polisi Tanzania ambao ulisogezwa mbele na bado haujapangiwa tarehe ya kuchezwa kabla ya kumalizana na Coastal Union.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Robertinho alisema: “Nashukuru Mungu kuona wachezaji wote wamerejea kikosini wakiwa salama kwa ajili ya kuendelea na programu za mazoezi ya kujiandaa na michezo yetu iliyosalia ya ligi lakini jambo zuri pia hata afya yao ya akili imeimarika baada ya mapumziko.

“Tumesahau yaliyopita na kama kikosi kwa sasa lazima tuhakikishe tunaanza upya kujenga timu ya ushindani ambayo itakuwa na uwezo wa kushindania ubingwa kwenye kila mashindano tutakayoshiriki msimu ujao.”

Stori na Joel Thomas

Leave A Reply