The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kushutumiwa na UN, Tanzania Yaikana Korea Kaskazini

0
Rais John Magufuli.

SERIKALI ya Tanzania imesema imeshtushwa baada ya kuorodheshwa miongoni mwa nchi za Bara la Afrika ambazo zimechunguzwa na Umoja wa Mataifa na kuhusishwa kuwa na uhusiano wa kibiashara na Korea Kaskazini inayoongozwa na Rais Kim Jong Yung.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana Ijumaa, Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Augustine Mahiga, alisema licha ya uhusiano uliokuwepo awali, lakini tangu mwaka 2014, Tanzania imepunguza kabisa uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia na nchi hiyo.

“Tulipopata taarifa kuwa kuna meli za Korea Kaskazini bado zinapeperusha bendelea ya Tanzania, tulizifutia usajili na bendera hizo zikashushwa, hata UN tuliwataarifu.

Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Augustine Mahiga.

“Hatuna ugomvi na Korea Kaskazini, lakini kitendo chao cha kutengeneza silaha za kuangamiza si kizuri kwa heshima na usalama duniani. Ndiyo maana tukaanza kuchukua hizo hatua za kupunguza mahusiano hayo,” amesema Dr Mahiga.

Mahiga aliongeza kuwa, uhusiano huo wa kibiashara ulikuwepo kabla ya vikwazo vilivyowekwa hivi karibuni na Baraza la Umoja wa Mataifa.

Waziri huyo amesema anaelekea katika mkutano wa kawaida wa Umoja wa Mataifa, ambapo atatumia fursa hiyo kujibu tuhuma hizo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong Yung.

Nchi nyingine za Afrika ambazo zinazochunguzwa na Umoja wa Matiafa kwa tuhuma za kwenda kinyume na vikwazo vilivyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja huo dhidi ya Korea Kaskazini ni Angola, Congo, Eritrea, Mozambique, Namibia, Uganda na Syria.

Ripoti ya uchunguzi huo ilitolewa Septemba 9, 2017. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema linachunguza tuhuma za Tanzania kuingia mikataba ya kijeshi na Korea Kaskazini inayogharimu dola za Marekani milioni 12.5.

VIDEO: Waziri Mkuu Awatumia Salamu Watu Wasiojulikana

Leave A Reply