Baada ya Kutua Mazembe, Ambokile Aanza Nyodo

MARA baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu ya kuichezea TP Mazembe, mshambuliaji Mtanzania, Eliud Ambokile amefunguka kuwa hiyo ni njia kwake ya kwenda kucheza soka la kulipwa Ulaya.

 

Ambokile alijiunga na Mazembe hivi karibuni akisaini dau la Sh mil 50 akitokea Mbeya City iliyokubali kumuachia ili ajiunge na klabu hiyo kubwa Afrika akichukua nafasi ya Ibrahim Ajibu wa Yanga.

 

Akizungumza na Chanmpioni, Ambokile alisema kuwa, nafasi hiyo aliyopata ataitumia vema kujitangaza kimataifa ili kufikia malengo yake aliyojiwekea.

 

Ambokile alisema ataanza majukumu kwenye kikosi cha Mazembe kwenye michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika mapema Julai, mwaka huu huko nchini Rwanda.

 

“Mazembe ni kati ya klabu kubwa Afrika yenye historia kubwa ya kuchukua makombe mengi likiwemo la Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo ni anafasi yangu kuitumia vema kujitangaza kimataifa zaidi.

 

“Nimepanga kujitangaza kwa kuhakikisha ninatimiza majukumu yangu yote ya ndani ya uwanja na kikubwa ni kufunga na kutengeneza nafasi za kufunga mabao.

 

“Ninataka kuona ninafika mbali ndani ya muda mfupi nikiwa na Mazembe kama alivyokuwa Samatta (Mbwana) anayeichezea Genk ya Ubelgiji,” alisema Ambokile.


Loading...

Toa comment