BAADA YA MONDI, DAVIDO YUPO NA CHRIS BROWN

SITAKI kuamini sana kuwa eti kwa sababu ameza-liwa Atlanta, Georgia nchini Marekani ndiyo maana ana kismati hivi!

Umri wake wa miaka 26 unanifanya bado nisiendelee kuamini kuwa mwanzoni mwa mwaka huu aliweza kukusanya kijiji cha Wazungu 20,000 pale kwenye Uwanja wa 02 Arena nchini Uingereza, karibia wote wakanyoosha simu zao na kumulika juu kama ishara ya kumkubali.

Kama ulikuwa hujui namzungumzia nani ni David Adeleke najua wewe unamfahamu zaidi kwa jina la Davido. Jamaa mmoja hivi aliyewahi kuja Bongo katika Tamasha la Fiesta 2014 akitokea kwao nchini Nigeria ambapo alikuwa ameandamana na msanii mwenzake, Tekno Miles.

Davido ndiye msanii wa kwanza kumshika mkono staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na kumvusha kimataifa kupitia Ngoma ya My Number One Remix na hii ilitokea baada ya kukutanishwa na mkali wa ‘commercial’, Ambwene Yessayah ‘AY’.

Licha ya kujiw-ekea heshima kubwa nchini Nigeria, Davido anabaki kuwa msanii mwenye mafanikio kibao kwenye muziki wake na katika makala haya yanachambua rekodi zake kwa uchache.

MKWANJA

Kwa mujibu wa Jarida la Forbes la Marekani la mwaka huu ambalo liliwataja wasanii wanaongoza kwa mkwanja barani Afrika, jina la Davido lilikuwepo.

Jarida hilo lilimtaja mkali huyu ambaye pia ni mmiliki na muanzilishi wa Lebo ya Davido Music Worldwide (DMW) kuwa utajiri wake unatokana na kupata madili tofauti, kusaini lebo kubwa ya muziki ya Sony pamoja na kufanya matamasha makubwa na mastaa mbalimbali.

Utajiri wake ulitajwa kufikia Dola za Kimarekani milioni 16 (zaidi ya shilingi bilioni 36).

KOLABO

Hadi sasa Davido anashikilia kobalo si chini ya kumi na kati ya hizo ni Fans Mi aliyomshirikisha rapa kutoka Marekani, Meek Mill. Ana kolabo ya Ngoma ya Beautiful aliyoshirikishwa na Kundi la Clean Bandit kutoka Uingereza.

Kolabo zake nyingine ni kutoka kwa memba wa Kundi la Migos, Quavo ambaye ameshirikishwa kwenye ngoma yake ya Swing na Way Too Fly akiwa na A Boogie wit da Hoodie.

Kwa sasa mkali huyu amesha-onesha mwaka kuwa yupo mbioni kuachia kolabo ya Ngoma ya Blow My Mind akiwa na staa wa R&B kutoka Marekani, Chris Brown. Mdogo-mdogo muziki wa Afrika unazidi kutoboa duniani. Big up!

 


Loading...

Toa comment