The House of Favourite Newspapers

Baada ya Mwanaye Kukondeana, Mama Wema Ataja Wauaji wa Mwanaye

0

VUNJA ukimya! Mama wa mwigizaji Wema Isaac Sepetu, Mariam Sepetu amevunja ukimya na kuwataka wale wanaojadili kukonda kwa binti yake, waache, kwa sababu ndiyo wanaoweza kumpa presha itakayomsababishia kifo, IJUMAA WIKIENDA lina habari kamili.

 

HUYU HAPA MAMA

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, mama huyo alisema kuwa, Wema alipokuwa mnene walimsema mno kuwa amekuwa mnene sana na hata sasa hivi amepungua, wameanza kumsema tena mtoto wake, mpaka anapata presha kwa ajili ya midomo yao, kitu ambacho hapendi kuona mtoto wake anapitia wakati mgumu kama ilivyo kwa sasa.

 

“Yaani mimi ningeomba sana wamuache mtoto wangu, maana wameshamsema sana, lakini bado tu hawajachoka, kama ni rahisi kumsema mtoto wa mwenzako kila kukicha, basi wajaribu upande wao maana mtoto wangu mpaka anapata presha kwa maneno yao na hao ndiyo wauaji wenyewe wa mwanangu,” alisema bi mkubwa huyo. ..

 

AUKUBALI MWILI WA SASA

Mama huyo aliongeza kuwa, yeye kwa upande wake anaona mwili wa mtoto wake uko sawa kabisa, hivyo watu wasimjadili kila wakati, kwani hakufanya kosa kuzaa mtoto ambaye ni staa.

 

“Mwili alionao hivi sasa ninaupenda, hivyo watu wasimchanganye hata kidogo, maana maneno yao yanampa presha mwanangu, yaani sipendi kusikia hata kidogo wakimsema mtoto wangu kwa chochote. Wamuache aendelee na kazi zake, maana sasa anafanya maisha yake,” alisema mama Wema.

 

NINI KIMEMKONDESHA?

Majibu ni mengi kuzidi swali lenyewe kiasi cha kufanya afya yake kuleta wingu zito miongoni mwa mashabiki wake. Imeelezwa mara kadhaa kuwa, kukonda kwa msanii huyo, kumetokana na upasuaji wa kukatwa utumbo aliofayiwa nchini India wenye lengo la kumfanya apungue baada ya kunenepeana.

 

MAJIBU YAKE…

Hata hivyo, mwenyewe amekuwa akisema hali hiyo inatokana na msongo wa mawazo unaotokana na mambo ya kimapenzi.

Ingawa wembamba siyo ugonjwa, lakini historia ya “kufungashia” aliyonayo msanii huyo, huwenda ndiyo inayomtesa, kwani wengi wamekuwa wakimtazama kwa mtazamo hasi. mifupa,” aliandika mwingine kwenye mtandao wa kijamii.

 

TUJIKUMBUSHE

Februari 4, mwaka jana, kupitia mahojiano maalum na mwandishi wetu kuhusu kukonda kwake, msanii huyo alisema; “Yaani hujui tu ninavyoufurahia huu mwili wangu wa sasa, nimekuwa siyo mzito tena, navaa nguo ambazo nazitaka na ninapendeza zaidi tofauti na ilivyokuwa huko nyuma, kwa kifupi najipenda hivi nilivyo.”

 

Ingawa mrembo huyo anasema anajipenda jinsi alivyo, wanaompenda zaidi bado wanatatizika na kukonda kwake. Mara kadhaa kumekuwa kukienezwa taarifa zisizokuwa na ukweli kwamba, Wema amekuwa akidondoka na kupoteza fahamu, huku kukonda kwake kukihusishwa na hali hiyo. Hata hivyo, mwenyewe amekuwa akikana kutokewa na hali hiyo na kusisitiza kwamba yuko sawa kiafya.

 

MAELEZO YA DAKTARI

Daktari Fredrik Mashili kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili, amewahi kuwaonya watu wanaotumia dawa kwa lengo la kupunguza miili yao na kuwataka wawe makini.

“Baadhi ya watu wanatumia dawa za kupunguza uzito bila kupata ushauri wa wataalamu, pia sina uhakika sana ila dawa nyingi za kupunguza uzito nchini kwetu hazijapata vibali, nyingi ni dawa za “Jamani hivi huyu dada ana tatizo gani, wembamba huu siyo bure, kimbunga kikipita si kinaondoka naye,” aliandika mtu mmoja kwenye Mtandao wa Instagram ambako picha ya Wema ‘aliyekonda’ ilipostiwa.

 

ANACHUKIA KUAMBIWA KAKONDA

Hata hivyo, msanii huyo amekua akikerwa na kauli za “umekonda” ambapo mara kadhaa amekuwa akiwajibu vibaya mashabiki wake wanaomsema hivyo.

UBONGE UNAPENDWA…

Katika kuonesha kwamba watu wanampenda “Wema bonge nyanya” wengi wao wamekuwa wakitafsiri kukonda kwake na tatizo la kiafya, kiasi cha kutamani arudie mwili wake wa zamani.

 

“Wema wa zamani alikuwa akipita mtaani, watu wanajipanga foleni kumshangaa jinsi alivyokuwa kafungashia. “Leo wakitoka watamshangaa jinsi alivyokonda na kubaki mtaani ambapo kiukweli zingine si dawa za uhakika au zinatumia njia ambazo si sahihi.

“Kuna watu wanazitumia na kuona kuwa wanapungua mwili kumbe wana sinyaa na hivyo kuwa katika hatari ya kupata matatizo ya kiafya,” Dokta Mashili anasema.

 

Uchunguzi unaonesha kuwa, Wema amekuwa akizidi kupungua kadiri siku zinavyozidi kwenda, jambo ambalo linawafanya watu wapate hofu juu ya afya yake. Agosti 2, mwaka jana kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wema aliandika hivi: “Daaaaah kutokana na comments za watu wengi, inaonekana wengi wanasema ninenepe tena jamani… Ila si ni nyinyi mlonisema nimekuwa Boooooongeee na ilibidi nipungue…

Leo nimeamini Binaadam hamna jema. “Anyways, I will soon Share The Secret to my weight loss na Msijali nitajitahidi kula kula kidogo ili niongezeke hata kidogo tu… Just so you know nilikuwa nina 109kgs na sasa nina 68kgs.”

 

Hayo ni maneno ya Wema mwaka jana lakini kwa kipimo cha macho kisichokuwa na uhakika, huwenda msanii huyo amepungua zaidi ya alivyokuwa wakati anaandika komenti hiyo. Kipi cha kushika kuhusu kukonda kwa Wema, linabaki kuwa wingu, hakuna wa kulishika zaidi ya kulitazama jinsi linavyochukuliwa na upepo.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply