The House of Favourite Newspapers

Baada Ya Ngoma…Yanga Yatangaza Pigo Lingine

0
Donald Ngoma akimalizia kumwaga wino Jangwani.

BAADA ya kufanikiwa kumbakisha mshambuliaji wao Mzimbabwe, Donald Ngoma uongozi wa Yanga umetangaza pigo lingine linakuja kwenye moja ya klabu hapa nchini.

Kauli hiyo, imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usa­jili ya Yanga, Hussein Nyika iki­wa ni siku moja imepita tangu wafanikiwe jaribio la Ngoma kwenda kwa watani wao Simba iliyokuwa inamuwania vikali kwa ajili ya kumsajili.

Ngoma alikuwepo kwenye orodha ya wachezaji iliyokuwa inahitajika kwenye usajili wa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara

na Kombe la Shirikisho Af­rika, mwakani.

Akizungumza na Cham­pioni Ijumaa, Nyika al­isema bado hawajafunga usajili licha ya kuwasajili nyota watatu ambao ni Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Pius Busitwa na Ngoma hivyo wanaendelea kwa ajili kukamilisha ripoti ya kocha wao Mzambia, George Lwandamina.

Nyika amesema hivi sasa wapo kwenye ma­zungumzo na mchezaji mmoja muhimu ambaye amelificha jina akiamini kama wakifanikiwa kum­nasa, basi itakuwa imela­mba dume.

Aliongeza kuwa, baada ya kukamilisha usajili wa mchezo huyo ndani ya siku hizi mbili, basi atasafiri nje ya nchi kwa ajili ya kuka­milisha usajili wa kiungo mmoja mkabaji wa kimatai­fa anayecheza namba sita.

“Muda mchache kuan­zia leo (jana), kesho (Iju­maa) au keshokutwa tuta­wataarifu ni mchezaji gani tumemsajili kwenye moja ya klabu kubwa hapa nch­ini, ninaahidi hilo mimi na kamati yangu ya usajili.

“Baada ya kufanikiwa kum­sajili mchezaji huyo, basi haraka nitasafiri kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kum­fuata mchezaji mwingine wa kimataifa anayecheza nafasi ya kiungo mkabaji, hivyo subiri nitaweka wazi,” alisema Nyika.

Stori: Wilbert Molandi | Championi Ijumaa

Leave A Reply