The House of Favourite Newspapers

Baada ya Okwi Kusepa Simba, Manara Amwaga Povu Kama Lote

‘Hata kagere na kina Okwi wajuzi waliyasema haya haya…’ Siku hizi sijishughulishi tena na kujibu jibu makala zenye lengo la kuichafua klabu yetu, nimeacha kwa sababu moja tu, wakosoaji wetu ni wale wale na kwangu hawana jipya sababu tushawazoea na tunawajua tabia zao za kutaka wao waonekane ndio wajuzi zaidi wa soka kuliko Watanzania wote.
Lakini hili la upotoshwaji wa usajili wa Deo Kanda nimeona nilisemee japo kidogo ili niwakumbushe Wanasimba wenzangu kuhusu kebehi za Wanazengo hao walizozitoa baada ya usajili wa Mawaria kina Meddie Kagere na wenzie.
Nyote mnakumbuka kebehi na maneno ya wakosoaji wetu kabla ya msimu uliopita kuanza, waliandika Simba ni Shikamoo Jazz, timu ya wazee, haitafika kokote na maneno mengi ya kuonyesha klabu imefanya usajili wa hovyo sana. Na tuliambiwa hata raundi ya kwanza ya ligi ya Mabingwa Afrika hatuvuki!!
Utatu wa John Boko, Emmanuel Okwi na Meddie Kagere ulipondwa hadi na mikongojo, yupo mmoja aliandika Simba inajifanyia dhambi yenyewe kwa kusajili vibabu vilivyojichokea!!
Uhhh lalaaah!! Nikiwauliza baada ya msimu kuisha ni  utatu upi uliokuwa bora ktk msimu uliopita wa ligi kuu kuwazidi hao wazee, sijui kama watanijibu!!
Idadi tu ya magoli waliyoyafunga msimu uliopita kwa pamoja ni rekodi isiyoguswa na washambuliaji wowote wale kabla na baada ya uhuru!!
Kagere ambae alikuwa mfano wa vibabu akawa top score wa ligi kuu, na kiukweli ndio best player wa ligi yetu ilioisha!!
Wanazengo hao wajuaji pia waliiponda sana beki yetu chini ya Pascal Wawa na Erasto Nyoni, lakini hao ndio mabeki walioruhusu magoli machache mno Kwenye ligi kuu ya msimu uliopita.
Leo watu wale wale ‘wajuaji ‘kwa nia ile ile na dhamira zao zile zile wanasema Deo kanda ni mzee na kutoa sababu zao zisizo na chembe ya ufahamu wa soka bali ujuzi wa kishabiki usioshabihiana na uhalisia wa mambo!!
Eti kanda alikuja Taifa na timu ya Congo miaka kumi iliopita hvyo hawezi kuwa na uwezo ule ule aliokuwa nao mwanzo!! Yesu wangu!! Hv hii football tunayoiandikia tunaijua au tunaichukulia poa tu?
Miaka kumi iliyopita ndio Simba ilimsajili Emmanuel Okwi ambae bwana mjuzi kamsifu kwa kucheza vzuri Kule Misri Kwenye Afcon, lakini hapo hapo anahoji kama kanda ataweza kuwa na ubora wa kumrithi Okwi ambae alimuona miaka kumi hiyo hiyo nyuma!!
Cha kushangaza Okwi huyu huyu waliemwita mhenga leo anapambwa kwa kuonekana ni bora sana sababu anaondoka Simba!! Hawa ndio watu wetu ambao hujui hata malengo ya maandishi yao wanayoyabatiza majina makubwa ili kuhalalisha tenzi zao!!!
Halaf anahoji why kama ana uwezo hayupo ktk team ya taifa? Lakini hakuwahi kuhoji kuhusu kutokuwepo kwa kina Makasu uwanjani au kutoitwa kwa Makambo ambae ni mshambuliaji mwenye uwezo na umri mdogo!!
Hv hafahamu Kupata nafasi Congo Kwenye timu ya taifa ni tofauti na Uganda au Tanzania? Anajua sana ila hapa anatupa dhamira yake kutuonyesha Simba na uongozi wake hawana wajualo ktk mpira ila yy na wenzie ndio wajuzi wa huu mchezo murua zaid duniani!!
Labda nimfahamishe yy na ww msomaji wa makala hii fupi, Deo Kanda alikuwa na ugomvi binafsi na kocha na akasema auzwe,Simba ikapeleka ofa TP Mazembe lakini Klabu hiyo ikagoma kutuuzia ila ikakubali kumleta kwetu kwa mkopo,na hii peke yake inathibitisha ubora wa Nyota huyo mwenye uzoefu mkubwa wa kusukuma gozi la Ng’ombe.
Na nimjuilishe pia dua lake la eti Simba itashindwa kuanzia pale ilipoishia msimu uliopita litaishia juu ya Dari, tumesajili kwa ufundi na mapendekezo ya benchi letu la ufundi na pia kwa kuzingatia matakwa na matarajio ya klabu Kwenye msimu ujao wa ligi.
Klabu yetu haisajili kwa presha ya ‘Wachambuzi’ inasajili kwa matakwa yetu na kwa ushauri wa wataalamu kweli wa soka,ndio maana kinatoka kitu (Okwi) kinakuja kitu (Kanda).
Nimalizie kwa kuwaambia wajuzi hiki sio kipindi cha kutuvuruga na kuwachanganya Washabiki wetu ambao tunajitahidi kuwahenga henga, so hatutakaa kimya kwa yoyote yule ambae tunadhani anataka  kutugombanisha uongozi wa klabu na Wanachama pamoja na Washabiki wetu!!
Endeleeni kumjadili Haji, klabu yetu iacheni, Simba haiwezi kuchezewa chezewa kwa kisingizio cha uhuru wa mawazo, na ikiwa hivyo mkubali mawazo yenu kupingwa hadharani!!
Na Haji Manara 

HISTORIA YA OPERATION ENTEBBE (Part 1)

HISTORIA YA OPERATION ENTEBBE (Part 1)

Comments are closed.