The House of Favourite Newspapers

Baada ya Shilole, Linah Naye Afungukia Kuhusu Ndoa Yake

 

Kwetu uchapa kazi na umahiri…

Tunatupilia mbali hofu, haikwamishi…

Twaendelea na kazi kwa ujasiri…

Na inatupa thamani, inayostaili…

Malkia wangu wa nguvu, Jasiri…

Mchapa kazi, mbunifu, Jasiri…

MALKIA wa Nguvu ni miongoni mwa ngoma zilizowahi kutikisha kunako Bongo Fleva kutoka kwa mwanadada, Esterlina Sanga ‘Linah’, ukipenda waweza kumuita Ndege Mnana.

Linah ni miongoni mwa wasanii zao la Jumba la Kuibua Vipaji (THT) ambaye amewahi kubamba na ngoma kibao ikiwemo Wrong Number akiwa na Barnaba, Raha Jipe Mwenyewe, Mtima Wangu akiwa na Amini pamoja na Hello akiwa na Christian Bella.

Juzikati Linah alitinga kwa mara ya kwanza kwenye mjengo mpya wa Global Group, Sinza-Mori jijini Dar na kuacha bonge moja la exclusive interview na katika makala haya yanaanika zaidi;

 

Over Ze Weekend: Kwa muda mrefu hujatoa ngoma, shida ni nini?

Linah: Nilikuwa kwenye uzazi jamani…na nimetumia karibu mwaka kubeba mimba na kujifungua na kulea, sasa imefikia hatua f’lani ya malezi ambayo sasa ninaweza kufanya kazi.

 

Over Ze Weekend: Ulijisikiaje wakati wengine wakiwa kazini, wewe ulikuwa kimya?

Linah: Kweli ilikuwa inaniuma, lakini sikuwa na jinsi. Niliamini tu kuwa kipaji bado ninacho na tena uwezo umeongezeka baada ya kupumzika kwa muda mrefu.

Over Ze Weekend: Una kazi ambayo umeshaifanya?

Linah: Kwa sasa nimeshafanya kazi nyingi ikiwa ni pamoja na video na nitakuwa ninatoa moja baada ya nyingine kwa hiyo nitarudi kwa sapraizi.

 

Over Ze Weekend: Utaratibu wa kuachia ngoma zako utakuwaje?

Linah: Sitakuwa kama watu wanavyofanya. Kwanza nitaweka makava kisha itafuatia video kamili, itakuwa staili ya kitofauti.

Over Ze Weekend: Linah wa zamani alikuwa mwembamba, lakini sasa hivi mnene, hii hali ukipita mtaani unajisikiaje?

 

Linah: Uzuri kila mtu anajua sababu ni uzazi na nimeipokea. Kama nikiichukia itanifanya nimchukie mtoto wangu, lakini pia komenti nyingi za mashabiki wangu ni za kunipongeza kwa muonekano wangu wa sasa.

Over Ze Weekend: Hutamani kurudia umbo lako la zamani?

Linah: Sidhani. Hata kama nitarudi vile, ujue kuna umri wa utoto na ukubwa, sasa nimepata umri wa ukubwa, kwa hiyo kama nikija kupungua itakuwa kidogo.

 

Over Ze Weekend: Tungependa kujua baada ya kujifungua, je, unaishi mwenyewe au na baba mtoto wako?

Linah: Mimi ninaishi mwenyewe, nipo mbali na baba wa mtoto wangu, lakini huwa anakuja kunitembelea na mwanangu.

 

Over Ze Weekend: Hivi karibuni ulikuwa kwenye harusi ya Shilole, je, upande wako umejipangaje?

Linah: Haya mambo ni Mungu mwenyewe, hata Shilole tulikuwa hatujui kama angeolewa hiyo juzi, ni wakati tu ulifika kwa hiyo kwa upande wangu siwezi kujipangia japo jambo hilo lipo na napenda kuolewa na baba wa mtoto wangu.

Sijapanga kuzaazaa nje na watu tofauti, ningependa watoto wangu wote wawe na baba huyohuyo labda kuwe na sababu nyingine kubwa sana, lakini so far tupo mbioni.

Over Ze Wekeend: Unakwepaje suala la skendo?

 

Linah: Hakuna mtu ambaye hana skendo kabisa hasa kwa sisi watu maarufu, huo ni uongo. Kuna zile zinatokea bahati mbaya, unaweza kuzuia, lakini huwezi kukuta ninafanya zile za makusudi.

Over Ze Weekend: Vipi suala la kuchepuka ulishawahi?

Linah: (anacheka) suala la kuchepuka kwangu no!

Over Ze Weekend: Ikitokea umejua baba mtoto wako amechepuka utafanyaje?

Linah: Hiyo itakuwa ni siri yangu mimi na yeye. Siku zote kwa wanawake waliokua na kufundwa huwezi kumuacha mumeo labda uwe na mambo yako mengine ya nje. Itabidi upambane na hali yako.

 

Over Ze Weekend: Mzazi mwenzako anakuchukuliaje ukivaa nusu utupu?

Linah: Kwanza aliniambia nifanye kitu ninachoona kipo sawa kwa faida yangu, lakini kisizidi, niwe katikati. Hajawahi kunifokea kwani amenikuta nikiwa ninavaa vinguo hivyohivyo kwa hiyo vitu vingine ninajiongeza tu, sasa hivi mimi ni mama, najua nifanye vipi niendane na hali hii.

Over Ze Weekend: Wimbo gani wa Aslay unaoukubali?

Linah: Ni huu alioimba kama rege unaitwa Pusha.

Over Ze Weekend: Tutegemee project gani kubwa?

 

Linah: Mwanzoni nilisema itakuwa sapraiz, lakini acha tu niseme, kuna project ninayokuja nayo na Recho (Kizunguzungu) japo siruhusiwi kuiimba ila inaitwa Same Boy, naomba mashabiki wetu waipokee kwani tukifuatilia hata komenti nyingi bado watu wanampenda na wanammis Recho so nilimtafuta na hata interview mbalimbali ninaongozana naye kwani nimetoka naye mbali tangu enzi za THT.

 

Mahojiano haya yanapatikana pia katika Mtandao wa Youtube kupitia Global TV Online unachotakiwa kufanya ingia Youtube kisha tafuta Global TV Online u-subscribe bila kusahau kubonyeza kengele pembeni yake na kushuhudia interview hii na nyingine kibao.

NA ANDREW CARLOS | Over Ze Wekeend | IJUMAA WIKIENDA.

 

Tamko la JPM Lamtesa Linah

Comments are closed.