The House of Favourite Newspapers

Baada ya Simba Kupewa Kichapo na Azam Hizi Ndizo Kejeli za Watani Wao wa Jadi Mitandaoni

  simba-4 JANA usiku Januari 14, 2017 kulikuwa na mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi uliopigwa kwenye uwanja wa amaan, Zanzibar kati ya Simba SC na Azam FC, mchezo ambao uliisha kwa Azam FC kufanikiwa kutwaa kombe hilo kwa kuifunga Simba SC bao 1-0, bao pekee lililofungwa na kiungo Himid Mao mnamo dakika ya 13 ya mchezo huo.

simba-9Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa kuwania kufuzu kuingia hatua ya nusu fainali ya kombe hilo, Yanga wapokea kichapo cha bao 4-0 kutoka kwa Azam FC licha ya timu zote mbili kufuzu na kuingia hatua hiyo.

simba-3Katika hatua ya nusu fainali Yanga alikutana mtani wake wa jadi, Simba siku ya Jumanne na Simba kufanikiwa kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kutoka suluhu ndani dakika 90 za uwanjani hivyo kuwaondoa kwenye mashindano hayo.

simba-11Baada ya kipigo hicho Yanga walishambuliwa mitandaoni na watani wao wa jadi (Simba) kwa kipigo hicho na kile cha Azam kilichopewa jina la 4G.

simba-12Kufuatia kipigo cha jana cha Simba kutoka kwa Azam, baadhi ya mashabiki wa watani wao wa jadi Yanga wamekuwa wakiwatania mitandaoni kwa kuweka picha za aina mbalimbali za kuwakejeri kutokana na kipigo hicho.simba-1

simba-8

simba-2

simba-10

Zicheki mwenyewe.

Comments are closed.