The House of Favourite Newspapers

Baada ya Tetesi za Kuhama, Hatimaye Juuko Arejea Upya Simba

0
Juuko Murshid akiwa na Hans Pope.

KLABU ya Simba imeendelea kumalika zaidi baada ya beki wake Mganda, Juuko Murshid kuungana na wenzake tayari kwa maandalizi ya mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.

Hiyo ni habari njema kwa kocha wa Simba na mashabiki kutokana na uwezo na mchango wa Mganda huyo aliounyesha katika msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara.

Mwishoni mwa msimu Juuko alihusishwa na kutaka kuondoka Simba na kutimkia Afrika Kusini kujiunga na  Orlando Pirates  ambayo kwa sasa inanolewa na kocha wa zamani wa Uganda, Milutin Sredojevic ‘Micho’.

 

Mratibu wa Simba, Abbas Ali alisema walikuwa  na lengo la kumuuza Juuko kwa Orlando, lakini  klabu hiyo haikuwa na nia ya dhati kwani tangu beki  alipofikia Afrika Kusini hajawahi hata kufanya mazoezi na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.

Abbas alisema jina la Juuko lilipendekezwa  nakocha Micho aliyekuwa naye katika timu ya Taifa ya Uganda, lakini mabosi wa Orlando hawakuwa na lengo la kusajili beki kwa sasa.

 

“Juuko mkataba wake unamalizika katikati ya msimu huu, lakini Micho alipopata kazi katika timu hiyo ya Orlando alipendekeza jina lake ili asajiliwe, lakini mabosi wa timu hiyo walitaka afanye kwanza majaribio na kama watalizika naye ndio wamsajili katika kikosi chao,” alisema.

“Tangu alipofika nchini humu hakufanikiwa kufanya mazoezi na timu hiyo hata siku moja, na ndio maana tumemwambia arudi nchini ikiwa kujiunga na timu yake kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi na mashindano mingine na kama kweli wanamuhitaji watamfuata tena,” alisema Abbas.  

Leave A Reply