Sanchi Aibuka Kivingine Siku ya Kuzaliwa Baada ya Ukimya

Mrembo maarufu nchini Tanzania, Surraiya Rimoy anayefahamika zaidi kwa jina la Sanchi, leo Juni 24, 2025, ameibuka mitandaoni kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa namna ya kipekee. Sanchi alipata umaarufu mkubwa kutokana na umbile lake la kipekee linalovutia macho ya wengi.
Baada ya kuwa ukimya bila kushiriki machapisho yoyote kwenye mitandao ya kijamii, Sanchi leo amewashtua mashabiki wake kwa kuposti picha mpya zinazoonyesha muonekano wake wa kuvutia, huku akiambatanisha na ujumbe wa kugusa moyo unaoashiria shukrani na matumaini mapya.
Kupitia chapisho hilo, Sanchi aliandika:
“Happy Birthday to Me 😍😍😍
Counting my blessings with a grateful Heart 🤗🤗
New 365 days of Massive Abundance await 🤩
To Live, Laugh and Love ❤️ #24June #Cancerian ♋️ 1111 ✅”
Ujumbe huo umeonesha kuwa mrembo huyo anaingia katika mwaka mwingine wa maisha akiwa na moyo wa shukrani, matumaini ya mafanikio, furaha, na upendo.

Mara baada ya kuposti, mashabiki wake waliendelea kumiminika kwenye sehemu ya maoni kwa kumtakia heri ya kuzaliwa, wakimsifu kwa uzuri wake wa asili pamoja na maneno yake yenye mvuto wa kiroho.
Sanchi ameendelea kuwa moja ya watu maarufu wanaovutia mashabiki wengi mitandaoni, si tu kwa mwonekano wake wa kipekee, bali pia kwa namna anavyojieleza na kujithamini.


Comments are closed.