The House of Favourite Newspapers

Baadhi ya Sababu Zilizomfanya Donald Trump Kushinda

donald-trump-wants-to-wage-economic-war-on-mexico-to-get-them-to-pay-for-a-border-wallMAREKANI: ALIYEKUWA mgombea urais wa Chama cha Republican nchini Marekani, amefanikiwa kushinda nafasi hiyo dhidi ya mgombea wa Chama cha Democratic,  Hillary Clinton, katika uchaguzi ambao ulifanyika tangu juzi na matokeo yake kutolewa leo.

Mwanzoni mgombea huyo alikuwa hapewi fursa ya kushinda nafasi hiyo na yeye mwenyewe alifikiri ingekuwa vigumu kushinda, lakini yote hayo yamefanyika na sasa ni rais mteule wa Marekani.

Davidson-MikePenceandtheTrumpVeepSweeps-1200Ushindi mkubwa ameupata katika majimbo ya Ohio, Florida na Carolina Kaskazini, maeneo ambayo yalikuwa chini ya ushawishi wa Clinton.

 Katika maeneo ya magharibi ya kati ya nchi hiyo ambayo ndiyo mama huyo angepata ushindi mkubwa, watu wa tabaka la wafanyakazi ambao wengi ni wazungu, hususan ambao hawana elimu, wanaume kwa wanawake, walikinyima kura chama hicho na kumwacha mgombea huyo mwanamke akipata kura chache.

Hii ni pamoja na wapiga kura wa vijijini ambao waliona serikali imekuwa ikipuuza maslahi yao.  Pamoja na kwamba majimbo ya Virginia na Colorado yalimpa kura nyingi mama huyo, jimbo la Wisconsin lilichukuliwa na kambi ya Trump na kuzidi kupunguza mategemeo ya Clinton.

Pamoja na kwamba Trump alikumbwa na matukio kadhaa mengi ambayo yalitishia kumnyima kura kama vile kutukana mkongwe wa vita, John McCain, kugombana na shirika la Fox News na mtangazaji wake, Megyn Kelly, pamoja na kashfa zilizodaiwa alizifanya dhidi ya wanawake, lakini huenda mvuto wake ulikuwa na nguvu kubwa na kumfanya yote hayo yasimletee madhara katika kupata kura.

Trump alionyesha nguvu kubwa dhidi ya chama cha Democrats na ndani ya chama chake ambapo watu mashuhuri katika chama hichokama Marco Rubio, Ted Cruz, Chris Christie na Ben Carson walibidi kushirikiana naye.

Vilevile, kilichokuwa kiwe kashfa ya kumpunguzia kura Clinton ambapo Mkurugenzi wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) alisema angefufua barua ya kufungua mashitaka dhidi ya mama huyo kwa kupitishia barua za serikali kwenye barua-pepe yake baadaye kiliachwa.

Lakini, hicho pia kilitosha kumdhuru katika uchaguzi kwani kilikuwa kimetokea karibu mno na mchakato wa kupiga kura.

Mabadiliko hayo na mengine, yalizidi kumuimarisha Trump ambapo aliweza kuwarudisha wenzake katika kumuunga mkono, na wakati huohuo kuyaathiri vibaya matumaini ya Clinton kwani suala la barua-pepe lilileta taathira kubwa kwake.

NA WALUSANGA NDAKI NA MTANDAO

Comments are closed.