Wakati wadau mbalimbali na wanatetezi wa haki za binadamu wakiwa wanazilalamikia kanuni mpya za maudhui mitandaoni ambazo zimetolewa hivi karibuni, bado wapo wadau wanaosema si kanuni zote zenye matatizo kwani kuna kanuni zingine ambazo zinalinda maadili na utu.
Vipengele hivyo vinahusu kulinda haki za mtoto, kuzuia matusi mtandaoni na hata kupunguza picha zisizofaa.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na wadau mbalimbali wakati wakichangia mdahalo ulioandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za binadamu (LHRC) uliokuwa na lengo la kujadili mchango wa mitandao ya kijamii katika kukuza utawala bora.
Comments are closed.