Baba Aitaja Nafasi ya Sure Boy Yanga

BABA mzazi wa kiungo wa Azam FC, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’, mzee Aboubakar Salum ‘Sure Boy Sr’ ameweka
wazi kuwa mtoto wake yupo
mbioni kumalizana na mabosi wa Yanga baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuvunja mkataba wa mchezaji huyo na Azam FC kutokana na mgogoro uliokuwepo.


Kiungo huyo ni miongoni mwa
wachezaji watatu wa Azam FC waliosimamishwa kwa utovu wa
nidhamu. Wengine ni Agrey Morris
na Mudathir Yahya.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, mzee Aboubakar alisema mtoto wake amebakisha asilimia chache za kujiunga na Yanga baada ya kufikia makubaliano kwenye mambo mengi ya msingi huku akienda mbali akisema tayari mkataba wake na Azam umeshavunjwa na TFF.


“Nilianza kusikia kwenye
vyombo vya habari lakini tayari kijana mwenyewe amenieleza kila kitu juu ya Yanga, tayari wameshakubaliana vitu vingi na mabosi wa Yanga kwa ajili ya kusaini mkataba baada ya TFF kuuvunja mkataba wake na Azam kutokana na mgogoro wao wa muda mrefu.


“Nadhani kwa sasa watakuwa
wamebakisha mambo machache ya kimasilahi kabla ya kumalizana kabisa, suala ya yeye kwenda kwenye timu ambayo nilicheza kwangu ni jambo zuri japokuwa sikutaka iwe hivyo, ila kutokana na
matatizo yake na Azam imekuwa ni
jambo kubwa.


“Yanga kuna wachezaji wengi
wazuri, suala la yeye kucheza itategemea na mwalimu atatumia mfumo gani, ila naamini atacheza tu,” alisema Sure Boy Sr.

Stori na IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam705
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment